Benki ya NMB imefadhili michezo ya UMITASHUMTA katika Manispaa ya
Sumbawanga kwa kutoa vifaa vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 9.
Lengo kuu la ufadhili huo ni kusaidiana na UMITASHUMTA katika kuibua na
kuendeleza vipaji vya michezo kwa shule
za msingi nchini Tanzania.
Meneja
wa NMB Tawi la Sumbawanga, John Chinguku (kuli) akimkabidhi Afisa
Elimu, Modesta Zambi, sehemu ya vifaa vya michezo vitakavyotumika
kwenye michezo ya UMITASHUMTA katika Manispaa ya
Sumbawanga. Makabidhiano hayo yalifanyika hivi karibuni kwenye manispaa
hiyo.
Maofisa wa Benki ya NMB na maofisa wa Manispaa ya Sumbawanga
wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Sumbawanga, John Chinguku (tatu
kulia) wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa hivyo vya
michezo.
Sehemu ya mipira iliyotolewa na Benki ya NMB kwa ajili ya UMITASHUMTA.
Post a Comment