Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Nukuu 5 za Serikali kuhusu zawadi kwa atakaefanikisha Mtuhumiwa bomu la Arusha kukamatwa na mengine


.
.Zifuatazo ni nukuu za maneno yaliyotolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, sera, uratibu na bunge William Lukuvi kuhusu hilo bomu ambalo lililipuliwa kwenye mkutano cha Chadema Arusha.
“Mtu asiejulikana alirusha kitu katika kundi la watu kilichosababisha mlipuko mkubwa, mkutano huu ulikua na ulinzi wa jeshi la Polisi wakiwa na magari mawili… askari walisimama upande wa Kaskazini ya uwanja ambapo mrushaji alikua mashariki na alirusha bomu kuelekea Magharibi”
“Jaribio la Askari Polisi kutaka kumfata alierusha lilizuiwa na makundi ya Wananchi ambao walianza kuwashambulia polisi kwa mawe na kuwazomea na hivyo Polisi kulazimika kuanza kujiokoa badala ya kumsaka Muhalifu”
“Mlipuko huo ulisababisha watu wawili kufariki dunia ambao ni Judith William (48) na mtoto Ramadhan Juma (15) na watu 70 wamejeruhiwa miongoni mwao watatu wamejeruhiwa vibaya na wawili hali zao ni mbaya”
“Uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa mlipuko huo ulikuwa ni wa bomu la kurusha kwa mkono ambapo pia aina ya urushaji wa bomu hilo haitofautiani na mbinu iliyotumika kwenye shambulio jingine la bomu lililotokea kwenye kanisa la Olasiti Arusha”
“Kutokana na mfululizo wa matukio haya mageni, Serikali imeamua kutenga shilingi milioni 100 kama zawadi kwa mtu yeyote atakaeshirikiana na kutoa taarifa zitakazofanikisha kunaswa kwa muhalifu wa matukio ya aina hii na mtandao wake mzima”

 
 
 
 
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top