Katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Mbinga Anastasia Amasi akionyesha sehemu iliyoanzia moto kuwaka na kukamata pazia.
Katibu
wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Mbinga Anastasia Amasi anayeonekana
katika picha akitoa maelezo kwa nje ambapo walimwaga mafuta aina ya
petroli dirishani na kuwasha moto.
Kama unavyoona katika picha hapo ni ndani ya ofisi baada ya moto kuwaka.
Huu ni mlango uliomwagiwa mafuta katika upenyo kisha kuwashamoto ambao haukuleta madhara kama walivyo kusudiwa na wachomaji.
Katibu
wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Mbinga Anastasia Amasi akizungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake ambao hawapo pichani.
--
Watu
wasiojulikana wamechoma moto jengo la ofisi ya Chama cha Mapinduzi
wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma tukio lililotokea Juni 21 mwaka huu
majira ya usiku pamoja mlinzi wa ofisi hizo kuwepo katika eneo hilo la
ofisi mpaka majira ya saa 12 asubhi na hakuweza kutambua kutokea kwa
kitendo hicho kilichofanywa na watu wasiojulikana usiku huo.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Mbinga
Anastasia Amasi amesema kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Juni
21 mwaka huu ambapo watu wasiojulikana walichoma moto moja ya jengo la
ofisi za chama hicho wilayani humo moto ambao ulielekelezwa katika
chumba cha ofisi ya katibu ambapo walivunja vioo na kuchoma moto mapazia
lakini kabla hawajachoma vitu vilivyokuwemo ndani walikimbia na kuacha
dumu lililokutwa likiwa na mafuta aina ya petroli.
Alisema
kuwa mpaka sasa hakuna hisia zozote zinazohusiana na tukio hilo ingawa
uongozi wa chama cha mapinduzi wilayani humo umeshatoa taarifa kwenye
vyombo ya ulinzi na usalama ambavyo vinaendelea na uchunguzi wa tukio
hilo.
Katika
hatua nyingine hali ya sintofahamu imejitokeza katika uchaguzi wa
viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga baada ya halmashauri hiyo
kugawanywa na kuzaliwa kwa halmashauri mpya ya wilaya Nyasa kwa kuibuka
kwa vitendo vya hujuma vinavyodaiwa kufanywa dhidi ya mgombea mmoja wa
nafasi ya mwenyekiti jina lake kuenguliwa katika mazingira ya
kutatanisha na kuzua maswali mengi miongoni mwa madiwani wa halmashauri
pamoja na wananchi na kutaka uchaguzi huo usifanyike mpaka majina yote
matatu ya wagombea yawepo.
Mmoja
wa wananchi wa halmashauri hiyo ya wilaya ya Mbinga ambaye pia ni
katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi wa kata ya Mbinga mjini Monika
John alisema kuwa hizo ni dalili za kuwepo kwa njama za wazi za kupanga
safu ya uongozi ambao siyo chaguo la walio wengi bali ni chaguo la
baadhi ya viongozi wa halmashauri hiyo kwa masilahi yao.
Akizungumzia
hali hiyo katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mbinga alisema kuwa
uteuzi wa wagombea wa nafasi hizo hufanywa kwa kuzingatia kanuni za
chama na wenye jukumu la mwisho la uteuzi ni uongozi wa chama ngazi ya
mkoa na yeye si msemaji wa maamuzi ya ngazi mkoa ingawa amepokea tarifa
ya kusitishwa kwa uchaguzi huo mpaka taarifa nyingine itakapotolewa na
ofisi ya chama ngazi ya mkoa.
Picha na Habari kwa hisani ya demashonews
Post a Comment