Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

OMMY DIMPOZ ALIPONZWA KWA KUSEMA UKWELI WA MOYONI JUKWAANI

 


Na Robert Maugo, Dodoma
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Ommy Dimpoz, akikwepa moja ya kopo la Bia lililorushwa na shabiki jukwaani hapo wakati akishambulia jukwaa wakati wa Tamasha la Kilimanjaro Tanzania Music Tour, 'Kikwetu Kwetu', lililofanyika jana kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, ikiwa ni shoo ya kwanza ya muendelezo wa Tour ya wasanii walioshiriki kwenye kinyang'anyiro cha Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013, zilizomalizika hivi karibuni nchini.

Ommy, wakati akipanda jukwaani hapo aliuteka umati wa mashabiki walioripuka kumshangilia kwa makelele kibao, lakini alichafua hali ya hewa pale aliposimama na kuanza kuzungumzia tukio lake aliloripotiwa na moja ya gazeti sikun za hivi karibuni lililomripoti kuwa alintusi marehemu Albert Mangwea.

Alianza kwa kusema, Jamani Naomba mnielewe mimi siwezi kumtukana Albert Mangwea, Yule ni Kaka yangu, na ninamheshimu sana ila naamini nilishindwa kueleweka tu na kukaririwa tofauti, hata yeye huko aliko anajua kuwa mimi sikumtukana na mungu anajua, nampenda sana na ninamheshimu sana na pia nawapenda sana mashabiki.

Baada ya kumaliza kauli yake hiyo, alianza kuwarusha mashabiki kwa vibao vyake vinavyoeleweka na wengi huku wengine wakishangili, na wengine wakitukana na kuzomea na pia wengine wakirusha makopo ya Bia ya Castle jukwaani kumtwanga nayo wakimtaka kushuka jukwaani hapo, jambo lililowafanya waandaaji kuwaamulu mabaunsa kumshusha jukwaani ghafla na wacheza shoo wake na kuacha muziki wake ukiendelea kurindima bila yeye jukwaani na baadaye kuzimwa na Dj, ambaye alikuwa hajafahamu kinachoendelea.

Baada ya kushuka jukwaani Dimpoz, alisikika akijilaumu kwa kuelezea ukweli wake wa moyoni, huku akisema kuwa, ''Najua nimewaudhi sana mashabiki wangu, lakini mimi nilikuwa naelezea ukweli wangu kutoka moyoni, na sitaacha kueleza ukweli ili watu wanielewe kuwa mimi sikuwa na nia ya kumtusi rafiki yangu, Kaka yangu, Marehemu Mangwea, Kiukweli nilijisikia kuwaeleza ukweli mashabiki kwani niliona pale ndiyo ningeweza kueleweka zaidi kutokana na umati mkubwa uliokuwapo eneo lile, lakini nao pia walinipokea tofauti, ila naamini ipo siku nitaeleweka na watu wataujua ukweli'', alisema Dimpoz
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top