Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

PINDA ATAMANI LETECIA NYERERE ARUDI CCM

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA.


LETECIA NYERERE




WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema anatamani siku moja Mbunge wa Viti Maalumu, Leticia Nyerere (CHADEMA) arudi Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Pinda alitoa kauli hiyo jana jioni wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Sumbawanga ng’ara kilichoandikwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Stella Manyanya (CCM), ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.

 

Hafla hiyo ya uzinduzi ilifanyika katika hoteli ya Dodoma na kuhudhuriwa na Mawaziri, Manaibu Mawaziri, viongozi kutoka Mkoa wa Rukwa, viongozi wengine wa Chama na Serikali.




Leticia Nyerere baada ya kuinuka ili kutoa salamu zake ndipo Waziri Mkuu Pinda aliposema kuwa anatamani siku moja Mbunge huyo wa Upinzani arudi CCM.


“Natamani siku moja urudi CCM,” alisema Waziri Mkuu.



Hata hivyo baada ya Mbunge huyo kufika mbele na kupewa kipaza sauti alisema ‘peoples power’ salamu ambayo hutumiwa na chama cha Chadema, hali iliyofanya watu waliokuwa ukumbini hapo kushindwa kujibu salamu hiyo na kubaki wakiangua kicheko.



Leticia alisema alikwenda pale kwa ajili ya kumuunga mkono Manyanya ambaye ni mwanamke kiongozi jasiri, ambaye mara nyingi amekuwa hasiti kuonesha ujasiri wake.


Alisema kuwa wabunge wanatakiwa kuonesha ushirikiano katika masuala ya maendeleo badala ya kuweka mbele itikadi za vyama.



“Tunapokuwa bungeni tunatakiwa tuwe wapinzani lakini tunapokuja katika suala la maendeleo tunatakiwa kuwa kitu kimoja,” alisema.



Leticia katika hafla hiyo aliongozana na watoto wake wawili wa kike wanaosoma Maryland, Marekani na Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipowaona aliwataka watoto hao kwenda mbele ili wasalimie.



“Hawa ni watoto wa Madaraka Nyerere, ni wajukuu wa hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere,” alisema Waziri Mkuu.


Alipouliza watoto hao wamefanana na nani, mmoja wa watoto hao alisema amefanana na bibi yake Maria Nyerere huku mwingine akisema amefanana na baba na mama yake.



Pia akitoa salamu zake, mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda alimpongeza Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Manyanya kwa juhudi anazofanya katika suala zima la kutunza mazingira.



Aliwataka wanawake wengine kuwa mstari wa mbele katika kuleta mabadiliko katika nyanja mbalimbali ikiwemo kujitosa kuwania Urais mwaka 2015.



“Kwa nini mwanamke asishinde Urais wa mwaka 2015 wao waweze wana nini na sisi tushindwe tuna nini,” alisema Mama Pinda
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top