Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RIDHIWANI KIKWETE NA MKEWE WAZUSHA TAFRANI NZITO .... RIPOTI KAMILI HII HAPA


MTOTO wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwan Kikwete na mkewe Arafa (pichani), wanadaiwa kuwaweka ndani wafanyakazi wao wa ndani kwa madai ya kuiba vitu mbalimbali vya ndani, ikiwamo ipad.

Baadhi ya vifaa vingine vilivyodaiwa kuibwa na wafanyakazi hao wa ndani ni pamoja na spea za gari, mashine ya kukamlia juisi na vingine ambavyo hata hivyo thamani yake haikuweza kujulikana mara moja.

Wafanyakazi waliokumbwa na tafrani hiyo na kusota katika mahabusu ya Kituo cha Polisi cha Oysterbay ni Halima Ramadhan, ambaye alikuwa akifanya kazi ya kulea watoto wa familia hiyo kwa zaidi ya miaka minne sasa na Sele Babu, ambaye alikuwa mpishi wa familia hiyo ya mtoto wa Rais Kikwete.

Habari zaidi zinasema kuwa wafanyakazi hao walifikishwa polisi na mke wa Ridhiwan, lakini taarifa hizo zilipomfikia Ridhiwan mwenyewe aliingilia kati kuwatoa kwa madai kuwa suala hilo lingechafua jina lake.

Akizungumza na gazeti hili kuhusu kufikishwa polisi kwa tuhuma za wizi huo, Sele Babu alikiri kuwapo kwa tukio hilo huku akisisitiza kuwa ni mambo binafsi kati yao na mwajiri wao, mke wa Ridhiwan, Arafa.

“Ni kweli tulifikishwa polisi, mimi ni mpishi na mwajii wetu ni mke wa Ridhiwan, suala la sisi kufikishwa ni mambo yetu binafsi na tulihojiwa na kisha kuachiwa,” alisema.

Alipobanwa kuwa alifikishwa polisi kwa madai ya wizi wa vifaa vya ndani vya familia ya Ridhiwan, Babu alikana kuhusika na wizi huo na kuongeza kuwa hata yeye amelisikia suala hilo kwa watu.

“Mimi nilikuwa likizo muda mrefu sijaenda pale nyumbani kwa Ridhiwan na hata jambo hili lilipotokea, nilipigiwa simu kuwa naitwa Polisi Oysterbay na nilipofika nikajieleza kisha nikarudi. Pale Polisi nilikuta jalada la wizi wa kuaminika. Hivyo suala la wizi lipo linasemwa, lakini zaidi aulizwe mwajiri wetu,” alisema Babu bila kufafanua wizi wa kuaminika ni juu ya kitu gani.


Tanzania Daima Jumapili lilipomtafuta mtuhumiwa wa pili katika tukio hilo, Halima, hakuweza kupatikana, lakini mwanae aliyejulikana kwa jina moja la Rogers, alikiri mama yake kufikishwa polisi kwa tuhuma za wizi huo.

“Mama amedhalilishwa sana kwa kuzushiwa wizi wa kitu kama ipad. Mama amekuwa akifanya kazi kwa zaidi ya miaka minne, huku akilea watoto na kazi nyingine lakini leo kupotea kwa vitu vidogo tu anadhalilishwa na kupelekwa polisi, hii si haki,” alisema Rogers.

“Tulipopata taarifa za mama kufikishwa polisi, tulikwenda nyumbani kwa Ridhiwan na tukaelezwa kuwa anashikiliwa polisi kwa wizi, hivyo tukafanya juhudi za kumwekea dhamana na tunashukuru ametoka,” alisema.

Kwa mujibu wa habari hizo, Halima amesimamishwa kazi katika nyumba hiyo ya mtoto wa rais, wakati Babu anaendelea na kazi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kinyela, alikiri kuwapo kwa tukio hilo, lakini hakuwa tayari kuzungumzia kwa undani.

Ridhiwan kwa upande wake, kupitia simu yake ya mkononi hakuweza kupatikana.

na Andrew Chale TANZANIA DAIMA
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top