Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Serikali kuzichukulia hatua kali halmashauri zisizotekeleza miradi ya maji

 


35530Na Gladness Mushi,Arusha SERIKALI  imeziagiza  halimashauri zote nchini  kuhakikisha zinakamiliza utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu ya miradi ya maji katika vijiji vitano ifikapo septemba  mwaka huu,na kwamba haitavumilia visingizio vya aina yoyote kwa halmashauri ambayo haitakuwa imekamiliza  ujenzi wa miradi hiyo.
Aidha  katika mwaka 2013/14 kila halimashauri imepewa jukumu la kukamilisha miradi mitano mingine kati ya 10 iliyopewa na kuzitaka ziwe zimetangaza zabuni za kutafuta wakandarasi wa ujenzi mapema ili
mradi wa vijiji 10 uwe umekamilika ifikapo juni 2014.
Kauli hiyo imetolewa mapema leo na waziri mkuu,Mizengo Pinda alipokuwa akifungua mkutano wa mwaka wa kujadili utekelezaji wa miradi ya maji vijijini unaofanyoka kwa siku tano jijini Arusha,ambapo zaidi ya
washiriki 500 kutoka sekta mbalimbali za  maji wamehudhulia.
Waziri Pinda alisema kuwa serikali haitasita kuchukua  hatua kali kwa wahandisi wa maji wa wilaya ambao hadi kufikia muda huo watakuwa hawajakamilisha  ujenzi wa miradi yote kwani hadi sasa halmashauri
zote zimeshapokea fedha zinazotesheleza ujenzi wa miradi yote mitano.
Hata hivyo alisema kwa kipindi cha miaka mitatu 2013-2016 serikali katika sekretarieti ya maji mapango huo unalenga kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji kwenye maeneo ya vijijini ,huku akisema hali hiyo ni kutokana na asilimia kubwa ya wananchi waishio vijijini  hawapati huduma ya maji ipasavyo kutokana na miradi mingi kuchakaa bila kukamilika kutokana na usiomamizi duni wa watendaji.
Mbali na hayo katika kutekeleza mradi huo itahitajika kiasi cha shilingi triolion 1.45 na utakapo kamilika kutakuwepo na uongezeko la wananchi milioni 15.5 waishio vijijini watakaopata huduma ya
maji,ambayo ni sawa na asilimia 74 ifikapao mwaka 2015 kutoka asilimia 57.
Awali akimkaribisha waziri mkuu, waziri wa maji Prof Jumanne Maghembe alisema katika mwaka 2013-2014 serikali imepanga kutekeleza miradi 1000 ya ujenzi wa  maji  mjini na vijijini utakao wanafaisha watu laki
8.7 kwa nchi nzima.
Aidha alisema  utekelezaji wa mpango huo unalenga kutekeleza mpango wa milennia ifikapo 2020 ili kuwanufaisha wananchi walio wengi hususani waishio vijijini  na kuwafikia kwa asilimia  62 ifikapo mwaka 2014.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top