Waziri
waNchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohd Aboud Mohd
kulia akibadilishana mawazo na Waziri wa Afya Juma Duni Haji nje ya
Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi mbweni nje ya mji wa Zanzibar. Muwakilishi
wa Jimbo La Mji Mkongwe Ismail Jussa Ladhu wakwanza kushoto
wakibadilishana mawazo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma
na Utawala bora Haji Omar Kheir katikati na Mwanasheria Mkuu wa Serikali
ya Zanzibar Othman Masoud Othman katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi
mbweni nje ya mji wa Zanzibar. Muwakilishi
wa Jimbo la Uzini Mohd Raza akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa
Thuwaiba Edington Kisasi wamwanzo kushoto na Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haji Omar Kheir wa mwanzo kulia
katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbweni nje ya mji wa Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI- HABARI MAELEZO ZANZIBAR.
Na Khadija Khamis – Maelezo Zanzibar 17/06/2013.
Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar imeeleza kuwa kasoro zinazojitokeza katika Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinapaswa kuingizwa na kujadiliwa
katika mchakato wa Katiba unaoendelea.
Hayo
yalielezwa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais
Muhammed Aboud Muhammed katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi, wakati
akijibu suala la Mwakilishi wa Jimbo la Wawi Saleh Nassour Juma
aliyetaka kujua vigenzo vya uteuzi wa Waziri Mkuu unaofanywa na Rais na
Zanzibar imetoa Mwaziri Wakuu wangapi tokea kuasisiwa Muungano.
Alisema
Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ambayo hadi sasa ndio
inayotuongoza haikueleza vigezo vya uteuzi wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania bali imetoa mamlaka ya uteuzi huo kwa Rais, na
tangu kuasisiwa kwa Muungano hadi sasa Zanzibar imetoa Waziri mkuu
mmoja ambae ni Salim Ahmed Salim.
Alifahamisha
kuwa tangu kuasisiwa kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Zanzibar
haijawahi kutoa Spika wala Naibu Spika isipokuwa imewahi kutoa
Mwenyekiti wa Bunge Zubeir Ali Maulid katika kipindi cha mwaka
2005/2010.
Hata hivyo
Waziri Aboud alisema kuwa nafasi bado ipo ya kuweza kueleza kero
zilizopo ambazo zinaonekana kwamba ni ukiukwaji wa Katiba ya Jamhuri ya
Muuungano ya Tanzania.
Alikiri kuwa
ipo hati ya makubaliano na maridhiano ya kikatiba kwa nchi zote mbili
zilizokuwa huru na mamlaka yake kamili na pia si kweli kuwa Zanzibar
haina wasomi .
Waziri
alieleza kuwa kero za Muungano bado zipo na ndio sababu moja wapo ya
kuanzisha mchakato wa katiba ili kuzitafutia ufumbuzi kero hizo.
Wajumbe wa
Baraza la Wawakilishi wamesema kuwa wanavyojuwa ni kua Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ni nchi moja kero zilizozopo zinafanywa kwa
makusudi.
Post a Comment