Sheha
wa Shehia ya Tomondo Mohd Omar Said { Kidevu } wakati alipokuwa
akipatiwa huduma za matibabu katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja kwa
takriban mwezi mmoja kabla ya kupelekwa Nchini India ambako ameanza
uchunguzi na matibabu zaidi. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
*****************************
Madaktari
Bingwa wa Hospitali ya Miot Mjini Chenai Nchini India leo wanaanza
kumfanyia huduma za matibabu Sheha wa shehia ya Tomondo Mohd Omar Said {
Kidevu } baada ya kukamilisha uchunguzi wa matatizo yake kufuatia
kumwagiwa Tindi kali karibu mwezi mmoja uliopita.
Sheha
Kidevu aliyefika Nchini humo Tarahe 21 na kufanyiwa vipimo vyote
vilivyohusika anaanza matibabu kwa hatua ya kupandikizwa ngozi katika
sehemu zake alizoathirika kutokana na kuungua kwa maji ya Tindi kali
hiyo.
Akizungumza
kwa njia ya Simu Daktari aliyeambatana na Sheha huyo Dr. Said Ali Said
{ Mkarafuu } alieleza kwamba Madaktari wa India wameelezea kuridhishwa
kwao na hatua kubwa iliyochukuliwa na Madaktari wa Zanzibar ya kumpatia
tiba sahihi mgonjwa huyo.
Dr.
Said alisema Madaktari hao Bingwa wa India wamekaririwa wakisema kwamba
wamepata matumaini ya huduma hizo alizofanyiwa Zanzibar ambazo zinawapa
hatua ya pili ya kuendelea na Tiba ya Sheha Kidevu.
“
Amefanyiwa uchunguzi wa vipimo vyote na kubainika kwamba jicho lake
Sheha Kidevu ambalo liliwahi kupata athari kidogo limewahiwa na
Madaktari wa Zanzibar wakiongozwa na Dr. Gang na Dr. Slim na hivi sasa
liko katika hali ya kawaida “. Alifafanua Dr. Said Mkarafuu.
Alifahamisha
kwamba Madaktari hao wa Hospitali ya Miot Mjini Chenai Nchini India
wameelezea matarajio yao kwa mgonjwa huyo kuendelea na huduma za
matibabu kwa haraka licha ya Madaktari hao kutokutaja huduma hizo
zitamalizika katika kipindi gani.
Kabla
Sheha Mohd Kidevu alikuwa akipatiwa huduma za matibabu katika Hospitali
Kuu ya Mnazi Mmoja kwa takriban Mwezi Mmoja sasa kutokana na
kuathirika sehemu ya kulia ya kifua chake, Bega pamoja na baadhi ya
maeneo ya mapaja.
Sheha
huyo wa Shehia ya Tomondo Mohd Omar Said Kidevu alipatwa na mtihani huo
wa kumwagiwa Tindi kali { Acid } na mtu asiyejuilikana Usiku wa tarehe
22 Mei Mwaka huu wa 2013 akiwa katika harakati za kuteka Maji mara
baada ya kurejea kwenye Ibada ya sala ya Ishaa.
Vitendo
vya matumizi mabaya ya tindikali vinavyofanywa na baadhi ya watu
vinaonekana kuanza kuwatia hofu wananchi na hasa baadhi ya Viongozi
katika maeneo mbali mbali hapa Zanzibar.
Post a Comment