MARIETHA NJIMBA (MRS. MZEE
MFAUME)
Familia
ya MZEE MFAUME na Wazazi Bw & Bibi CLAUDE NJIMBA wa Kinyerezi na Tabata Dar
es salaam wanapenda kutoa Shukrani kwa wote walioshiriki katika msiba wa mpendwa wao MARIETHA NJIMBA (MRS. MFAUME)
kilichotokea tarehe 29/05/2013 na kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni tarehe
01/06/2013.
Shukrani za pekee tunazipeleka kwa Uongozi na wafanyakazi
wote wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dr Kisanga, Dr Mary,
wauguzi wa Burhan Hospital, Mapadre na Waumini wa Parokia Katoliki ya Kinyerezi,
Kristu Mfalme – Tabata, Majirani, Ndugu,
Jamaa na Marafiki wote kwa jinsi mlivyoshirikiana nasi katika msiba huo.
Sio rahisi kuwataja kwa majina wote walioshiriki nasi. Tunaomba mzipokee
shukrani zetu kwa waraka huu.
Shukrani za kumaliza msiba huo zitafanyika nyumbani kwake
Kinyerezi, siku ya Jumamosi tarehe 06/07/2013 kuanzia 02 asubuhi kwa Ibada ya
Misa Takatifu nyumbani kwa Marehemu. Tunawakalibisha wote.
BWANA AMETOA NA
BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.
Post a Comment