DALADALA 95 zimekamatwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), kutokana na makosa mbalimbali, ikiwemo kutoza nauli kubwa kinyume na bei elekezi ya serikali.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Mfawidhi Kanda ya Mashariki Conrad Shio, alisema kukamatwa gari hizo, ni ushirikiano kati ya mamlaka hiyo na Jeshi la Polisi.
Alisema Daladala 41zilikamatwa kutokana na makosa ya kutoza nauli kubwa, 16 kuiba njia, 13 kukatisha njia, nane kugushi leseni, sita kwa matumizi ya lugha chafu kwa abiria na 11 kwa kutotoa tiketi au kutokuwa nazo kabisa.
Shio alisema daladala nane zilikamatwa kwa makosa ya kuiba njia, katisha njia na kuzidisha nauli, magari hayo yamesimamishwa kutoa huduma na SUMATRA inashikilia leseni zao kwa ajili ya kuzifungia kwani makosa yao yamekuwa yakijirudia mara kwa mara.
Alizitaja daladala hizo kuwa ni T182BXQ – T/Segerea – Temeke, T740BPN – Buguruni – Mvuti, T950BQT – Temeke – Chanika, T275BTU – Temeke – Chanika, T621BJD – Machimbo- Chanika, T807BMP – MB/R3 – Kilwa Masoko, T563BQC – Kigogo Fresh – Kariakoo, T965BZP – Buguruni – Mvuti.
“SUMATRA kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi tunaendelea kufanya msako wa daladala zinazovunja sheria na kanuni mbalimbali barabarani hasa makosa ya kutoza nauli kubwa, kuiba njia na kukatisha nji, hivyo wananchi tunaomba ushirikiano kwa kutuletea namba za magari yanayokiuka sheri”alisema Shi
Katika makosa yaliyoorodheshwa, ambayo ni kutoza nauli kubwa, kuiba njia, kukatisha njia na lugha chafu, mamlaka hiyo imetoa masharti yafuatayo lazima yatimizwe; Mmiliki anatakiwa kuchapisha nauli halali na kuziwasilisha SUMATRA, kuwasilisha mkataba wa dereva mwingine badala ya dereva aliyeingia naye makataba wa awali (kwa makosa yote manne), Kuandika barua ya kutokurudia tena kosa, kulipa faini kwa makosa aliyokamatwa na
Credits: Fullshangwe
Post a Comment