Kocha wa Taifa
Stars, Kim Poulsen ameiita tena kambini timu hiyo Julai 4 mwaka huu kujiandaa
kwa mechi ya kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani
(CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.
Taifa Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inavunja kambi leo (Juni 17 mwaka
huu) baada ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia, kundi C Kanda ya Africa dhidi
ya Ivory Coast iliyochezwa jana (Juni 16 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Kim amesema
wachezaji watakaoitwa kambin ni wote walioko kwenye timu hivi sasa isipokuwa
Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaocheza mpira nchini Jamhuri ya Kidemokrasi
ya Congo (DRC) katika klabu ya TP Mazembe Englebert.
Wachezaji hao
ni Juma Kaseja, Aishi Manula, Aggrey Morris, Mwadini Ally, Ally Mustafa, Shomari
Kapombe, Kevin Yondani, Erasto Nyoni, Haroub Nadir, Mwinyi Kazimoto, Frank
Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Simon Msuva,
John Bocco, Vicent Barnabas, Mudathiri Yahya, Athuman Idd, Haruni Chanongo na
Zahoro Pazi.
Mechi hiyo
namba 37 dhidi ya Uganda (The Cranes) itachezwa jijini Dar es Salaa kati ya
Julai 12 na 14 mwaka huu wakati ile ya marudiano itafanyika wiki mbili baadaye
katika Uwanja wa Mandela ulioko Namboole nje kidogo ya Jiji la
Kampala.
wakati huo
huo mchezo kati ya Taifa Stars dhidi ya Ivory Coast zaidi ya Shilingi Milioni
mia tano zilipatikana katika mchezo huo
Kutokana na
Tiketi za mechi hiyo kuuzwa kati ya Sh. 5,000, Sh. 7,000,
Mgawanyo wa
mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani
(VAT) ni sh. 76,596,254.24 wakati wa gharama za uchapaji tiketi ni sh.
7,809,104.
Asilimia 15 ya
uwanja sh. 62,658,846.26, asilimia 20 ya gharama za mechi sh. 83,545,128.35 na
asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh.
20,886,282.09.
Asilimia 60 ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 250,635,385.06 na Chama cha
Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 12,531,769.25 ambayo ni asilimia
5 kutoka kwenye mgawo wa TFF.
Mechi iliyopita ya Stars dhidi ya Morocco
(Lions of the Atlas) kwenye uwanja huo iliingiza sh. 226,546,000.
Post a Comment