Mratibu
Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou akizungumza wakati
wa maadhimisho ya siku ya Wakimbizi Dunia ambapo amesema anaishukuru
Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani katika kuhakikisha
Wakimbizi wanakuwa katika mikono salama ya Serikali ya Tanzania.
Kila
tarehe 20 ya mwezi Juni Dunia inatambua uwepo wa mamilioni ya Wakimbizi
Duniani katika kuhakikisha wanasaidiwa Ili kuondokana na hali ya
Ukimbizi katika nchi za ugenini.
Aliendelea
kusisitiza kwamba ni vigumu kuelewa Mazingira hatarishi ambayo mkimbizi
anayapata kutokana na mapigano ya kisiasa, kidini au kikabila ambayo
inawalazimisha kuhama katika makazi yao na kwenda katika makazi ambayo
hawayafahamu, alisema watu wasiokuwa na makazi wanazidi kuongezeka
Duniani mpaka 2012 takribani watu Milioni 3 walikuwa hawana makazi hizi
ni kengele za uamsho wa Jumuiya ya Kimataifa kuamka na kuchukua hatua.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Pereira A. Silima akizungumzia majukumu ya
Serikali katika kuwahudumia Wakimbizi kutoka nchi za jirani zenye
mapigano ya wenyewe kwa wenyewe katika siku ya Wakimbizi Duniani jijini
Dar es Salaam.
Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wakimbizi Duniani (UNHCR) Bi. Joyce
Mends-Cole akitoa nasaha zake ambapo amesema anatambua uwepo wa Shirika
la Wakimbizi nchini Tanzania katika kuendeleza kampeni ya 2011
inayozungumzia umuhimu wa mwamko wa matatizo ya wakimbizi Duniani.
"Sisi
Umoja wa Mataifa Tanzia tunasaidia kuhamasisha mwamko huo wa uelewa wa
matatizo ya Wakimbizi katika Dunia ya utandawazi ili jamii ijue majanga
na madhara ya vita katika familia na kaya".
Pia
ameongeza kuwa Shirika la Wakimbizi Duniani litaendelea kuelimisha
madhara ya vita katika nchi zinazoendelea ili kupunguza ongezeko la watu
wasiokuwa na Makazi Duniani.
Balozi
wa Marekani nchini Mh. Alfonso Lenhardt na Balozi mpya wa Tanzania
nchini Marekani Mh. Liberata Mulamula wakifuatilia hotuba mbalimbali
katika siku ya Wakimbizi Duniani iliyofanyika jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa Juma.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou na baadhi ya wageni waalikwa wakati wa maadhimisho hayo.
Pichani
Juu na Chini ni Wageni waalikwa na maafisa mbalimbali wa Umoja wa
Mataifa nchini wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakijiri wakati wa
maadhimisho hayo.
Post a Comment