NA SULEIMAN MSUYA
MSAJILI
wa Vyama Vya Siasa nchini John Tendwa amesema ili kuhakikisha kuwa
amani inaendelea kudumu ni muhimu kuwepo kwa uvumilivu na kuhueshimiana
kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA).
Kauli
hiyo ameitoa leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku
chache baada ya kutokea kwa mlifuko wa bomu kwenye mkutano wa kampeni ya
udiwani uliokuwa unaendeshwa na CHADEMA katika viwanja vya Soweto mjini
Arusha.
Tendwa
alisema kwa muda sasa kumekuwepo kwa msuguano mkubwa baina ya vyama
hivyo viwili jambo ambalo linaonyesha dalili za kuhatarisha amani ya
nchi na wananchi kwa ujumla.
Msajili
huyo alisema vyama hivyo vinaonyesha kukosa uvumilivu na kuheshimiana
kwani kwa kipindi hiki kifupi cha kampeni za udiwani viomekuwa na fujo
ambazo kila mmoja anamshutumu mwenzake jambo ambalo sio nzuri katika
nchi.
Alisema
kutokana na tukio hilo viongozi wao wameibuka na kushutumiana ambapo
Katibu Uenezi wa CCM Nape Mnauye alisikika akiwashutumu CHADEMA
kuhusikana wakati Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akisema CCM na
Jeshi la Polisi wanahusika.
“Inasikitisha
sana kuona watu wanakufa alafu watu wanajitokeza na kuanza kushutumiana
kuwa huyu ndiye anahusika mimi nomba wapeleke ushahidi Jeshi la Polisi
ili kuweza kusaidia upelelezi,” alisema.
Tendwa
alisema katika kuhakikisha kuwa vyama hivyo vinaendelea kuheshimiana na
kuvumiliana anatarajia kuita kikao ambacho kitashirkisha ofisi yake,
jeshi la polisi na vyama hivyo kwani wanapoelekea ni pabaya.
Alisema
iwapo uchaguzi wa Udiwani hali inakuwa hivyo je itakuwakuaje katika
uchaguzi wa Serikali za Mitaaa na uchaguzi mkuu watu watarajie nini
kwani ni ishara mbaya kwa Taifa ambalo linasifika kwa amani.
Aidha
Msajili huyo alipotakiwa kuelezea juu ya ofisi yake kuvifuta vyama
hivyo viwili vya CCM na CHADEMA alisema ofisi yake ina mamlaka hayo ila
hiyo ni hatua ya mwisho kuchukuliwa iwapo itabidi.
Tendwa
alisema uamuzi wa kuvifuta vyama hivyo unaweza kuwa na athari kubwa
kwani utahitaji gharama kubwa za kufanyika uchaguzi jambo ambalo sio la
kukimbilia.
Alisema
ofisi yake inahitaji kukutana na vyama hivyo kwani ndio njia sahihi ya
kufikia muafaka kwa maslahi ya vyama hivyo na wananchi kwa ujumla.
“Ni
lazima jamii itakatumbua kuwa maamuzi haya yanahusi CCM ambayo ipo
madarakani ambapo matokeo yake ni kuvunja Serikali na kwa CHADEMA ni
kuwaondoa wabunge wake hivyo uchaguzi kufanyika tena,” alisema.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini Peter Mziray
amevitaka vyama hivyo kutambua kuwa nchi hii iwapo itaingia vitani wao
ndio wahusika wakubwa.
Alisema
Baraza hilo linatajia kukutana kwa pamoja likishirikisha vyama vyote
vya siasa ambapo watatoka na azimio juu ya hali ilivyo hivi sasa kwani
inaonyesha dalili za kupotea kwa amani.
Mziray
ambaye ni Rais Mtendaji wa Chama cha African Progressive Party Tanzania
(APPT Maendeleo alisema hali inayotoke kwa sasa jeshi la Polisi na
vyombo vyote vya usalama vinapaswa kushutumiwa kwani vionyesha kutofanya
kazi vizuri.
Mwenyekiti
huyo alisema hali hiyo inasikitisha sana kutokana na ukweli kuwa watu
wasio na hatia kupoteza maisha jambo ambalo halikubaliki.
“Kwa
kweli vyama hivi viwili vimekuwa na matukio mbalimbali ambayo kwa muono
wangu nadhani vinahitajika kubadilika kwani hali sio shwari ila vyombo
vya usalama pia vina mapungufu yao,” alisema
Post a Comment