Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na
Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akiwa na Mjumbe wa Kamati
Kuu na Mwenyekiti wa Uhusiano wa Kimataifa wa Chama Cha Kimomunisti Cha
Viatnam (CPV), Hoang Binh Quan, baada ya ujumbe wa CPV kuwasili asubuhi
hii kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es
Salaam. Quan na ujumbe wake wanatarajiwa kuwa na mazungumzo na Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana baadaye leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa
CCM mkoa wa Dar es salaam, Ramadhani Madabiba.
Balozi wa Vietnam Tanzania,
NguyenThien akimtambulisha Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa
Uhusiano wa Kimataifa wa Chama Cha Kimomunisti Cha Viatnam (CPV), Hoang
Binh Quan kwa katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Martin
Shigela (kulia) baada ya kushuka katika ndege, kwenye Uwanja wa Ndege wa
Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Katibu wa NEC ya CCM, Uhusiano wa
Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akiwatambulisha kwa Mjumbe wa Kamati
Kuu na Mwenyekiti wa Uhusiano wa Kimataifa wa Chama Cha Kimomunisti Cha
Viatnam (CPV), Hoang Binh Quan, viongozi wa CCM aliofuatana nao katika
mapokezi hayo, wakiwa chumba cha mapumziko Uwanja wa Ndege wa JN.
Dk.Asha-Rose Migiro na mgeni
wake, wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa mgeni huyo na viongozi
wengine wa CCM, wakati wamapokezi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
JN, Dar es Salaam.
Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na
Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akizungumza na Mjumbe wa
Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Uhusiano wa Kimataifa wa Chama Cha
Kimomunisti Cha Viatnam (CPV), Hoang Binh Quan, baada ya kumpokea kwenye
Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere asubuhi hii. PICHA ZOTE NA BASHIUR NKOROMO
Post a Comment