WANAWAKE
wakiwezeshwa kiuchumi na kupatiwa elimu ya msingi ya ujasiriamali,
kuepuka maradhi hatarishi na kufahamu haki zao katika jamii, umasikini
utapungua, kipato kitaongezeka na maisha ya Watanzania yatabadilika.
Hayo
yalisemwa leo na Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa Kwa Wote (EOTF),
Mama Anna Mkapa wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya wanawake
wajasiriamali yanayoendelea kwenye ukumbi wa Bwalo la Maafisa la Jeshi
la Kujenga Taifa (JKT),Mgulani jijini Dar es salaam.
Mama
Anna Mkapa ambaye pia ni Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin
Mkapa alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa kiuchumi
na kijamii wajasiriamali hao kutoka mikoa yote Tanzania Bara na
Visiwani, ambapo jumla ya wanawake wapatao 264 wanashiriki.
“Mfuko
wa Fursa Sawa Kwa Wote umekusudia kwa nguvu zake zote kuendeleza vita
ya hii ya kuwawezesha wanawake nchini kujikwamua katika wimbi la
umasikini, maradhi na ujinga,” alisisitiza Mama Mkapa.
Aidha
ameiomba Serikali, Asasi za kiraia, taasisi za dini, wahisani binfasi
ndani na nje ya nchi, kusaidia wanawke haswa wa vijijini kujikwamua
na umasikini.
Mama
Mkapa aliongeza kuwa mfuko huo, kwa kipindi cha miaka 16 zaidi ya
wanawake 6,820 wamepata mafunzo ya stadi za biashara na wengine 4,500
wamepata fursa ya kushiriki maonyesho mbalimbali ya ndani na nje ya nchi
kwa kupitia EOTF ili kutangaza na kuuza bidhaa zao.
Naye
Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko Dk. Abdallah Kigoda akifungua
mafunzo hayo alisema Serikali imeanzisha utaratibu wa kuweka
kumbukumbu za mkopo katika mabenki kwa kupitia ‘Credit Reference Bureau’
ili kuweza kusaidia kuwafahamu wateja, na kuwaasa wajasiriamali
wanapokopa wakumbuke kulipa kwani uaminifu ni kitu muhimu katika
biashara.
“Suala
lingine la kulipa kipaumbele ni lile la kuongeza thamani ya mazao
wanayoyazalisha na tuache kuwazalishia watu wengine bidhaa wakaenda
kuongezea thamani kidogo tu kama vile kwa kufunga na kuweka nembo ya
kibiashara na kuuza kwa bei kubwa,” alisema Dk. Kigoda.
Aliahidi
kuwa Wizara yake iko makini kufanya linalowezekana kushirikiana na
wajasiliamali hao kutatua tatizo hilo la kuuza malighafi badala ya
bidhaa iliyoongezwa thamani ili kuongeza ajira na kupunguza umasikin
Post a Comment