Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WANNE WASEMEKANA KUFA AJALI YA MAGARI NA PIKIPIKI ILIYOTOKEA MVOMERO, MOROGORO

 




WATU wanne wanasemekana kufa kwenye ajali iliyotokea leo majira ya saa tatu asubuhi eneo la Bwawa la Hatari kijiji cha Dakawa Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro katika barabara kuu ya Morogoro-Dodoma.
 Ajari hiyo iliyohusisha magari matatu ambayo ni lori aina ya Scania, magari madogo mbili aina ya Prado na Noah, pikipiki ya matairi matatu 'Bajaj' na pikipiki ya matairi mawili aina ya Sanlg.
 Mashuhuda wa tukio hilo walidai kwamba watu wanne walikufa papohapo akiwemo dereva wa pikipiki ya matairi mawili.
 Mashuhuda walisema chanzo ni dereva wa Noah aliyejaribu kuzipita pikipiki mbili na lori moja na kwamba Noah hiyo iliyokuwa ikielekea Dodoma ilipojaribu kuipita Bajaj mbele aliona gari linakuja na kwamba alifunga breki ghafla na kusababisha dereva wa lori  iliyokuwa mbele yake  kuigonga pikipiki (bodaboda) iliyokuwa mbele yake.  Hivyo Noah hiyo ikaikumba Bajaj na kupinduka, ambapo lori  nalo lilihama njia na kwenda porini baada ya kujaribu kukwepa tukio hilo.
Hayo yalisemwa na  shuhuda mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Abdallah Shabani ambaye alikuwa akilima kandokando ya barabara hiyo.
chanzo:.globalpublisher
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top