Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WATANZANIA TUSIKWAZIKE KWA ULINZI MKALI WA RAIS OBAMA


Rais Obama akiwa katika ofisi yake angani.

ULINZI mkali ambao tayari upo na utazidi kuonekana wakati wa Ujio wa Rais wa Marekani umewafanya baadhi ya Watanzania kujihisi wanadunishwa au kuaibishwa. Wapo wengine ambao wanaona kuwa hatua mbalimbali za kiusalama zinazochukuliwa kumlinda Obama, familia yake na ujumbe wake zinaonesha dharau na kutoaminiwa kwa vyombo vyetu vya ulinzi. Wengine wanafika mahali pa kuhisi kuwa Wamarekani wanatudharau sana kiasi kwamba wanatuchagulia nani aonane na Obama (rejea taarifa kwenye gazeti la Mwananchi la leo). Watanzania hawapaswi kujisikia hivyo hata kidogo.

Ulinzi wa Obama ni Mkali iwe ndani ya Marekani au Nje

Wakati wowote Rais wa Marekani anaposafiri iwe ndani ya Marekani au nje ya Marekani ulinzi wake ni mkali na karibu kamili (almost absolute). Kuanzia anga ambalo anakuwepo (linakuwa no fly zone) na kuwa anaenda na kila kitu kinachoweza kutumika wakati wowote wa dharura yoyote inayoweza kufikirika kutokea. Kuanzia majanga ya moto, maji, maandamano ya kisiasa au hata mapinduzi ya kijeshi ulinzi wa Rais wa Marekani umejiandaa.

Mfano mzuri ni kuwa ikulu ya Rais pale DC – Jumba Jeupe – juu kabisa kuna mzinga wa kutungua ndege – surface to air battery. Lakini kubwa zaidi ni kuwa anga lote linalozunguka Ikulu hiyo ni eneo ambalo ndege haziruhusiwi kuruka (prohibited airspace). Na wakati wowote Rais anaposafiri mahali popote ndege haziruhusiwi kuruka juu yake. Anapotua kwenye uwanja kwa mfano Detroit, hakuna ndege nyingine itakuwa inatua wakati huo huo! Sasa kama hili linatokea Marekani, kwa kiasi gani linaweza kutokea Tanzania?

Ripoti hii maalum basi ina lengo la kuwasaidia Watanzania kutokwazika na kiasi cha ulinzi ambao Obama anakuja nao pamoja na usumbufu unaotokana na hilo. Kama msafara wa Rais Kikwete huwa unazusha usumbufu kwa watu basi wa Obama utasababisha kadhia – chukua msafara wa Kikwete zidisha mara 1000!

 

  
Mambo ya Kawaida ya Ulinzi wa Rais

Kwa yeye kuwa Rais wa Marekani Obama anapatiwa ulinzi wa hali ya juu kabisa labda wa kiongozi mwingine yeyote duniani. Anapokuwa ndani ya Marekani anapata bado ulinzi wa hali ya juu lakini pia ni kama mara ishirini hivi chini ya ulinzi anaopata akiwa nje ya Marekani. Hii ni kwa sababu moja kubwa anapokuwa Marekani anakuwa katika ulinzi wa vyombo vingi sana vya nyumbani na mahali popote anapokwenda. Hivyo, vitu kama magari watu, n.k vingi vinakuwa ‘mobilized’ kutoka ndani.

Ulinzi huu wa kawaida ni ule ambao mara nyingi watu wanaona (maafisa wa Usalama wanaoambatana na Obama popote anapokwenda) na ule ambao uko kwenye kivuli (usionekana) ambao unahusisha wataalamu wa mambo ya mawasiliano, wapelelezi, majasusi n.k

Rais wa Marekani anapotoka nje ya nchi anaenda pamoja na kikosi cha maaskari wasiopungua 500 hivi! Ulinzi wa Rais wetu huwa ni kama watu 40 hivi maafisa wa usalama na anapoenda nje namba hiyo inapungua kidogo. Tunaposema anakuja na watu 500 hivi kwa ajili ya ulinzi hawa ni nje ya wale wanaotangulia na wale ambao taifa husika linatoa. Kati ya hao walinzi kama 200 hivi ni makomandoo watupu wa jeshi la Marekani na Taasisi za kijasusi.

Rais Obama anaposafiri anasafiri na madaktari bingwa wasiopungua sita hivi pamoja na wapishi wake pamoja na choo chake! Pamoja na hao anaambatana na manesi na wataalamu mbalimbali wa afya ambao wanaweza kuingia kazini wakati wowote. Anapokuwa Washington DC hospitali moja iko maalum kwa ajili ya dharura ya Rais tu na ina mlango wake ambapo likitokea jambo basi Rais hatopata shida ya kuzungushwa! Pamoja na hivyo kuna kiasi cha lita za damu aina AB (damu ya Obama) ambayo pia inasafiri naye mahali popote kwa ajili ya dharura yoyote itakayohitaji kuwekewa damu. Hii ni ndani au nje ya Marekani.

Gari lake nalo ni chombo cha ulinzi 
Bila ya shaka katika ya vyombo vya ulinzi wa karibu kabisa kwa Rais ni gari lake analotumia ambalo limetengenezwa maalum kwa ajili ya kumpatia ulinzi wa hali ya juu. Hii ni pamoja na kuzuia risasi na milipuko ya mabomu ya mkono au rocket launcher! Na huwa hali moja bali kadhaa ili kuhakikisha watu hawajui Rais anakuwa katika gari gani hasa.


Kwa ripoti kamili soma hapa:
http://www.mwanakijiji.com/2013/06/ripoti-maalum-watanzania-wasikwazike-na-kufedheheka-kwa-ulinzi-mkali-wa-obama/
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top