Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WATU WATATU WAPOTEZA MAISHA KATIKA MATUKIO TOFAUTI SUMBAWANGA


IGP Mwema
Na Elizabeth Ntambala wa Matukiodaima.com ,Sumbawanga

WATU watatu wamekufa katika matukio tofauti likiwemo la
mwanaume kumuua mkewake na mtoto kwa kuwakata kata kwa kutumia panga.

Katika tukio la kwanza mwanaume aliyefahamika kwa jina la
Amos Ukiwa(33) alimuua mke wake Happy Lucas(25) pamoja na mtoto wake aitwaye
Bakari Ukiwa mwenye umri wa miaka mitano kutokana na wivu wa kimapenzi.

Tukio hilo lilitokea Juni 24 majira ya saa 5;30 za usiku
ambapo ulizuka ugomvi baina ya wanandoa hao ambapo mume alikuwa akimtuhumu mke
wake kuwa anauhusiano nje ya ndoa yao na mwanaume mwingine ambaye alidai kuwa
hata mtoto mdogo alienae alipata ujauzito kutoka kwa mawanaume huyo.

Kutokana na ugomvi huo wa kurushiana maneno ulisababisha
wanandoa hao kuanza kupigana ndipo kwa hasira Ukiwa alipoamua kuchukua panga na
kuanza kumkata mke wake hadi alipomuua na akamkata pia mtoto huyo naye hadi
akamuua na kisha kutorokea
kusikojulikana.

Katika tukio jingine Ligobert Senga(35) mkazi wa kitongoji
cha Kizwite Sumbawanga mjini alikutwa amekufa katika uwanja wa mpira wa
Sekondari ya Kizwite huku mwili wake ukiwa hauna jeraha lolote kuonesha kuwa
ameuwa.

Inadaiwa kuwa marehemu alifariki dunia kutokana na kudhoofu
sana afya yake ambapo alikuwa akinywa pombe kari bila kula chakula hali
iliyopelekea kudhoofu kwa afya na ndiyo sababu kubwa iliyochangia kifa chake.

Kamanda wa polisi mkoani Rukwa Jacob Mwaruanda amethibitisha
kutokea kwa matukio hayo yote na kuongeza kuwa mtuhumiwa wa mauaji ya mke wake
na mtoto amatafutwa atakapo kamatwa atafikishwa mahakamani.
mwisho
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top