Washindi wa Mashindano ya Guinness Football
Challenge 2013 wakiwa kjatika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni
ya Bia ya Serengeti (SBL) Epraimu Mafuru naMeneja wa bia ya Guinnes Davis Kambi wakati wa tafrija hiyo.
Regina Gwae kutoka kampuni ya R & R
Associate akizungumza jambo na mmoja wa washiriki wa mashindano ya Guinness
Football Challenge
Ilikuwa ni furaha tu kwa kila
mtu.
Meneja wa bia ya Guinness Davis Kambi (kushoto) na Mkurugenzi wa
Masoko wa SBL, Ephraim Mafuru wakiwa katika picha na wadau wengine wa Guinness
na wafanyakazi wa SBL.
Wadau wa Guinness wakibadilishana mawili matatu
wakati wa tafrija hiyo.
Baada ya kumalizika kwa mashindano ya Guinness Football Challenge
yaliyokuwa yakiendeshwa na Kupitia kipindi maarufu cha Guinness
Football Challenge TV Show, hatimaye wawakilishi wa Tanzania katika mashindano
hayo jana wamefanyiwa sherehe fupi katika Ukumbi wa Savannah Lounge Jijini Dar
es Salaam na waandaji na wadhamini wa shindano hilo Kampuni ya Bia
ya Serengeti kwa kuwapongeza kwa hatua
waliyofikia.
Yaliyokuwa yakifanyika Afrika Kusini hatimaye yalimalizika hivi
karibuni huku timu ya Tanzania ikiishia katika hatua ya nusu fainali kwa nchi
kadhaa za Afrika ikiwemo Ghana, Cameroon, Kenya na Uganda zilizoshiriki
mashindano hayo ukiwa ni msimu wa
tatu.
Katika hafla hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na wanahabari iliwashuhudia
vijana walioshiriki mashindano hayo wakiwa na nyuso za furaha na kulakiwa kwa
shangwe na uongozi wa Kampuni ya Bia ya
Serengeti.
Akizungumza katika hafla fupi iliyofanyika katika Ukumbi wa Savannah
Lounge Meneja Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti,Moses Kebba ameipongeza timu
hiyo kwa kufikia hatua nzuri ya mashindano hayo ambayo yalishirikisha timu
mbalimbali za nchi zingine za
Afrika.
Alisema kwamba katika hatua hiyo ya nusu fainali waliofikia ni
dhahiri vijana hao wamefanya kazi nzuri huku akivishukuru vyombo vya habari kwa
kuwatangaza vyema wakati wa ushiriki wao kati mashindano hayo ya Guinnes
Football Challenge.
Amesema kwamba katika mashindano hayo nchi kadhaa zilishiriki kama
vile Ghana, Cameroun, Kenya & Uganda, ambapo amekiri kwamba
katika mashindano hayo kumekuwapo na ushindani mkubwa licha ya Tanzania
kutoibuka na ushindi ilifanikiwa kufikia katika hatua ya nusu
fainali.
Kwa upende wake Meneja wa bia ya Guinnes Davis kambi amesema kwamba wataendelea kusaidia zaidi kuibua vipaji vya soka kupitia ushiriki huo ambao utaleta tija katika soka la Tanzania kwa kutangazika hatimaye kufanya vyema katika mashindano hayo ambayo yamekuwa na umaarufu mkubwa Afrika na sasa wataendelea kutafuta zaidi vipaji vitakavyoshiriki katika msimu ujao.
“Kila mmoja katika kampuni yetu ya SBL na watanzania wanayofuraha na
nakuwapongeza Daniel Msekwa na Mwalimu Akida, kwa
kufanya vizuri licha ya kushindwa kufika hatua ya fainali lakini kazi mlioifanya
imeonekana na mmeweza kuiwakilisha vyem Tanzania katika mashindano ya Guinness
Football Challenge”, Alisema Kambi
Katika fainali ya mashinado hayo yaliyoshirikisha pia timu za Uganda
na Kenya timu ya Tanzania ya GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE
iliwakilishwa na Daniel Msekwa, Mwalimu Akida, Mohamed Kobembe, Gullam Sosha,
Hamza Rashid,Lukwesa Kanakamfumu, Abubakari Mohamed, Kherry Sadallah, Simon
Chimbo na Emmanuel Temu.
Akizungumzia mashindano hayo Daniel Msekwa amesema: “Tumepata uzoefu mkubwa katika
mashindano lakini kubwa ni kuhakikisha tunafanya mambo kulingana na mawasiliano
ya kupata vipaji zaidi ambapo timu za Kenya na Uganda zilifanikiwa kufikia
malengo mazuri lakini hayo yote ni changamoto
kwetu.”
“Tunaishukuru Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa sababu
walifanya kila jitihada kipindi tupo Afrika Kusini kwenye mashindano na kuona
utofauti wa nchi zingine kama Ghana na Cameroon,
Post a Comment