Askari
Jamii wakiwa kwenye maandamo wakipita mbele ya mgeni rasmin hayupo
pichani, katika kilele cha Madhimisho ya wiki ya Safiri Salama, huko
katika kiwanja cha Polisi Mahonda.
Meneja
kitengo cha maradhi yasiyoambukiza Wizara ya Afya Zanzibar Omar Mwalim
Omar akitoa nasaha kwa madereva kupunguza ajali za makusudi, huko
Mahonda katika Madhimisho ya wiki ya Safiri Salama yaliodhaminiwa na
Wizara ya Afya na Jeshi la Polisi Zanzibar. Kamishna
wa Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa akiwahutubia wananchi katika
madhimisho ya wiki ya Safiri Salama, kulia Meneja kitengo cha maradhi
yasiyoambukiza Wizara ya Afya Zanzibar Omar Mwalim na kushoto Mkuu wa
Wilaya Mkoa wa Kaskazini (B) Khamia Jabir, huko katika kiwanja cha
Polisi Mahonda Mkoa wa Kaskazini (B).
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Na Salum Vuai, Maelezo
..Kaskazini Unguja yaongoza kwa ajali barabarani
WATU
52 wamepoteza maisha na wengine 332 wamejeruhiwa kutokana na ajali 175
za barabarani zilizotokea katika Mkoa wa Kaskazini Unguja kati ya
Januari mwaka 2011 hadi katikati ya mwaka 2013.
Takwimu
hizo zimetolewa jana na Mkuu wa Usalama Barabarani wa jeshi la Polisi
mkoani humo Ali Muhsin, wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya
‘Safiri Salama’, yaliyofanyika katika viwanja vya Mahonda, Wilaya ya
Kaskazini B.
Mkuu
huyo alisema, ajali za barabarani ni tishio kubwa kwa watumiaji wote
wa barabara, wakiwemo madereva, abiria na watembeao kwa miguu, na kwamba
tahadhari kubwa inahitaji kuchukuliwa kuziepuka.
Alieleza
kuwa, endapo watumiaji wa barabara hawatakuwa waangalifu, majanga ya
maafa, ulemavu wa kudumu, majeraha, hasara kwa mali na uharibifu wa
miundombinu, vitaendelea kuliandama taifa.
Alitaja
sababu mbalimbali zinazochangia ajali hizo, kuwa ni uhaba wa
miundombinu imara, ubovu wa vyombo vya moto, mabadiliko ya hali ya hewa,
utendaji mbaya wa wasimamizi wa sheria za usalama barabarani na kasoro
za kibinadamu.
Ili
kumaliza au kupunguza ajali za barabarani, Muhsin alisema hatua kadhaa
zinapaswa kuchukuliwa, ikiwemo kutoruhusu magari na vyombo vyengine
visiingizwe barabarani hadi vithibitishe kuwa na sifa kwa mujibu wa
sheria.
Aidha
alishauri vyombo vyenye majukumu ya kutoa huduma kwa umma na kusimamia
sheria kama vile polisi, mahakama, Idara ya Usafiri na Leseni, Bodi ya
Mapato Zanzibar na vyengine, vitekeleze majukumu yao kwa uadilifu na
uaminifu.
Kwa
upande wake, mgeni rasmi katika sherehe hizo Kamishna wa Polisi
Zanzibar Mussa Ali Mussa, alisema ajali za barabarani ndizo zinazoongoza
kwa kuua watu wengi, kuliko vifo vitokanavyo na sababu nyengine.
Alieleza, takwimu zinaonesha kuwa, takriban watu milioni moja na laki mbili hufariki kwa ajali hizo kila mwaka duniani kote.
Kwa
Zanzibar, alisema ajali 3869, zimeripotiwa kutokea kati ya mwaka 2009
hadi 2012, ambapo kati ya hizo, watu 450 walipoteza maisha, na 3855
walipata majeraha mbalimbali.
Kamishna
huyo aliongeza kuwa, kwa kipindi cha Januari hadi Machi mwaka 2013,
jumla ya ajali 196 zimeripotiwa, ambazo zimesababisha vifo vya watu 24
na majeruhi 258.
Aidha
alisema, ukiondoa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkoa wa Kaskazini Unguja
ndio unaoongoza kwa ajali nyingi za barabarani, kulinganisha na mikoa
mingine minne Unguja na Pemba.
Alifahamisha
kuwa, kwa kutambua uzito wa jambo hilo, Jeshi la Polisi kamisheni ya
Zanzibar, limekuwa likifanya jitihada mbalimbali kwa kushirikiana na
wadau wote wa matumizi ya barabara ili kuimarisha usalama wa watumiaji.
Aliwataja
wadau hao kuwa, ni jamii yote ya Zanzibar, taasisi za serikali na
binafsi, ikiwemo Bodi ya Mapato Zanzibar na Wizara ya Afya, ambayo
imeshirikiana kikamilifu na jeshi hilo kufanikisha wiki hiyo ya ‘Safiri
Salama’.
Hata
hivyo, alikumbusha kuwa, jukumu la kuhakikisha usalama wa barabarani la
jeshi la polisi pekee, bali ni la kila mmoja kwa nafasi yake, huku
akisisitiza matumizi mazuri ya barabara ikiweemo kuzitunza badala ya
kuziharibu kwa visingizio mbalimbali, pamoja na kung’oa vyuma vya alama
za barabarani.
Naye
Meneja wa kitengo cha maradhi yasiyoambukiza kutoka Wizara ya Afya Omar
Mwalimu, alisema hospitali kuu ya Mnazimmoja, imekuwa ikipokea majeruhi
na maiti wengi kutokana na athari za ajali za barabarani, na kusema
zinailazimu serikali kutumia fedha nyingi nje ya bajeti yake, kuwatibu
watu wanaopatwa na ajali.
Wiki
ya ‘Safiri Salama’ ilianza tarehe 24 Juni mwaka huu, kwa mikutano ya
kutoa elimu kwa watumiaji wa barabara, kama vile madereva na makondakta,
wanafunzi, mabagwani na wananchi wengine wa Mkoa wa Kaskazini.
Sherehe
hizo zilizopambwa kwa burudani mbalimbali zilizobeba ujumbe wa usalama
barabarani kutoka kwa kikundi cha Black Roots chini ya msanii Makombora
na utenzi, zilihudhuriwa pia na Wakuu wa Wilaya za Kaskazini B, Khamis
Jabir Makame na Riziki Juma Simai wa Kaskazini A, pamoja na makamada wa
Polisi wa mikoa mitatu ya Unguja
Post a Comment