MBUNGE
WA Kigoma Kaskazini, Ndugu Zitto Z. Kabwe amealikwa kuhudhuria tamasha
la tisa la Aspen la mwaka huu huko Marekani. Tamasha hilo linawaleta
pamoja watu mashuhuri kutoka nyanja mbalimbali duniani.
Lengo kubwa la tamasha ni kuwawezesha washiriki kubadilishana mawazo kuhusiana na masuala mbalimbali ambayo wana uzoefu nayo.
Ushiriki
katika tamasha hilo utamwezesha Zitto kukutana na kubadilishana mawazo
na magwiji wa masuaka mbalimbali duniani. Ratiba iliyotolewa na
waandaaji inaonyesha kuwa tamasha hilo litakaloendeshwa kwa muda wa wiki
moja kuanzia Juni 26, limegawanyika katika sehemu mbili.
Kama
ilivyo kwa miaka iliyopita, tamasha hilo litahusisha majadiliano ya
pamoja, ya vikundi pamoja na ya mtu mmoja mmoja. Pia washiriki watakuwa
na fursa ya kukutana na wabunifu na wataalamu wa nyanja mbalimbali na
kubadilishana nao mawazo.
Mijadala
itahusu mambo ya kijamii, siasa, mahusiano ya kimataifa, watoto na
vijana pamoja na namna ya kukabiliana na changamoto kubwa zinazoikabili
dunia hivi sasa.
Vile
vile kutakuwa na maonyesho ya vitabu pamoja na mikutano na waandishi wa
habari maarufu kutoka Marekani. Washiriki pia watapata fursa ya
kujifunza kupitia filamu na michezo ya kuigiza. “Nimefurahi kupata
mwaliko huu na nimekubali kushiriki kwa sababu kwangu mimi hii ni nafasi
adhimu sana na kupanua uelewa wangu wa masuala mbalimbali, pia ni fursa
kubwa ya kueleza maoni yangu kwa waalikwa mbali mbali.
Nina
uhakika kuwa watu nitakaokutana na kubadilishana nao mawazo na uzoefu
watasaidia kupanua uelewa wangu wa masuala kadhaa”, alisema Zitto
alipotakiwa kufafanua umuhimu wa tamasha hilo kwa vijana.
Baadhi
ya watu maarufu watakaotoa mada katika tamasha hilo ni pamoja na Majaji
washiriki wa Mahakama Kuu ya Marekani Stephen Breyer na Elena Kagan,
Mwakilishi Eric Cantor, Rais wa Kituo cha Brady Dan Gross, Rais wa Chama
cha Wamiliki wa Bunduki Marekani David Keene, Balozi wa Marekani katika
Umoja wa Mataifa Susan Rice; Rais wa Taasisi ya Taasisi ya Kulinda
Rasilimali, Frances Beinecke; Mkurugenzi mwenza wa Boies, Schiller &
Flexner LLP David Boies, Waziri wa kazi wa zamani Elaine Chao, Waziri
wa Usafirishaji Ray LaHood, Meya wa New Orleans Mitch Landrieu, Waziri
wa Fedha wa zamani Hank Paulson, Gavana wa zamani wa Minnesota Tim
Pawlenty, Mshauri wa Chama cha Republican Karl Rove na Rais wa
Shirikisho la Walimu Marekani Randi Weingarten.
Taasisi
ya Aspen inajihusisha na masuala ya elimu na sera ambayo ina makao
makuu katika jiji la Washington, Marekani. Lengo lake kuu ni kuendeleza
maadili ya kiuongozi. Pia taasisi hii ni kama kituo cha kuwezesha
kutafuta ufumbuzi wa masuala magumu.
Taasisi
ina matawi kadhaa baadhi yakiwa huko Aspen, Colorado na Wye River huko
Maryland. Pia Taasisi ina ofisi katika jiji la New York. Pia taasisi ina
mtandao mkubwa wa washiriki duniani kote.
Post a Comment