Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Askari JWTZ akamatwa na meno ya tembo ya bil 9


*Alitaka kuingia Malawi, apandishwa kizimbani
OFISA Uvuvi wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Suleiman Chesana, anayekabiliwa na kesi ya kukutwa na meno ya tembo yenye thamani ya Sh bilioni nne, amepandishwa tena kizimbani baada ya kukutwa na meno mengine ya tembo kilo 781 yenye thamani ya Sh bilioni 9.3.

Mshtakiwa huyo, alipandishwa tena kizimbani jana kwa mara nyingine katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mjini Dar es Salaam, mbele mbele ya Hakimu Sundi Fimbo na kusomewa mashtaka na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Tumaini Kweka.

Kweka alidai kosa la kwanza ni la kujishughulisha na nyara za Serikali bila kibali, kinyume na Sheria ya Uhujumu Uchumi.

Ilidaiwa Mei 23, mwaka huu, katika mpaka wa Malawi na Tanzania, mtuhumiwa alikamatwa akisafirisha isivyo halali nyara zenye thamani ya Sh bilioni 9.3, zikiwa zimefichwa katika mifuko ya saruji, wakidai wanasafirisha saruji.



Hata hivyo, Hakimu Fimbo alimtaka mshitakiwa asijibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo na kwamba Mahakama Kuu ya Tanzania, ndiyo yenye mamlaka ya kusikiliza.

“Mahakama inaahirisha kesi hii hadi Julai 20, mwaka huu, itakapokuja kwa ajili ya kutajwa na mshtakiwa arejeshwe gerezani,” alisema.

Julai 9, mwaka huu, mshitakiwa huyo, alifikishwa mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi, Nyigulile Mwaseba, akikabiliwa na kesi ya kukutwa na meno ya tembo yenye thamani ya Sh bilioni nne.

Wakati huo huo, mahakama hiyo ilishindwa kutoa uamuzi wa kumuona Johnson Lukaza na Mwesigwa Lukaza kama wana kesi ya kujibu au la kwa sababu hakimu mmoja katika jopo linalosikiliza kesi hiyo ni mgonjwa.

Hakimu Nyigulile Mwaseba, aliahirisha kesi ya wizi wa Sh bilioni sita hadi Julai 15, mwaka huu, ambapo jopo hilo litakuja kutoa uamuzi wake wa kuona washitakiwa hao kama wana kesi ya kujibu au la.

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top