* Atoweka nyumbani kwa siku mbili
Mwenyekiti wa Mtaa wa Ihanga Kata ya Ilomba Emanuel
Mwasibata akiwa amesimamia kikao cha usuruhishi
Dereva wa daladala Aswile Mwalukoba aliyeshika fimbo
baada ya kurejea nyumbani na kuhudhuria kikao cha usuruishi ambapo alikili
kuzaa na mwanafunzi huyo na kukubali kuzika .
Daladala iliyobeba mwili wa Marehemu kutoka
Uyole.
Wakazi wa Uyole wakiwa wameshikwa na butwaa baada
yakumkosa mwenyeji wao
Kulia ni Carolina Kyando akiwa na dada yake baada ya
kuleta mwili wa mtoto nyumbani kwa Mwalukoba eneo la Mama John jijini Mbeya
Majirani pande zote mbili wakingojea kujua hatma ya
mazungumzo yanayo endelea baada ya Mwalukoba kurejea
******************
Vitendo vya ukatili
dhidi ya watoto na wanawake jijini mbeya vimeendelea
chukua sura mpya baada ya dereva wa daladala jijini humo
kumzalisha mwanafunzi Masomo ya jioni kituo cha Juhudi kilichopo
Ilomba.
.
Tukio
hilo limetokea hivi karibuni eneo la mama John Mtaa wa Ihanga Kata
ya Ilomba ambapo dereva wa daladala aliyefahamika kwa jina la Aswile Mwalukoba
(45 ) kutelekezewa wa miezi saba ambaye alikwisha fariki baada ya kuugua kwa
muda mfupi.
Akizungumzia tukio hilo
Mwenyekiti Mtaa huo Ndugu Emanuel Mwasibata amesema kuwa mgogoro huo umetokana
na dereva huyo kugoma kuuzika mwili huo kwakile alicho dai kuwa
hivi sasa haishi na binti huyo kwa muda mrefu
sasa.
Kwa upande wake binti
huyo aliyefahamika kwa jina la Calorina Kyando amedai kuwa kitendo cha yeye
kuuchukua mwili wa mtoto huyo hadi kwa baba yake unatokana
kutelekezwa na bwana huyo kisha kupigwa marakwa mara na kusababishiwa
ulemavu wa sikio la kushoto baada ya kung’atwa na mwanaume
huyo.
Mwanamke huyo
amefafanua kuwa mara baada ya mtoto huyo kufariki wakati akipatiwa matibabu
katika Hospital ya Igawilo jijini humo aliamua kumpigia simu mzazi mwenzie kwa
lengo la kumpa taarifa za msiba huo.
Amesema mara baada ya
kutoa taarifa hiyo mwanaume huyo alikubali na kumueleza mwanamke huyo kuwa yuko
tayari kwa ajili ya mazikoya mtoto huyo ambapo anafanya taratibu za kuwasiliana
na ndugu zake walioko Tukuyu Wilayani Rungwe.
Amesema katika siku
iliyofuata mwanaume huyo hakupatikana kwa simu ya kiganjani na wala hakuwepo
nyumbani kwake anapo ishi eneo la Mama John hali iliyo plelekea baadhi ya
majirani na mwanamke huyo kutoka Uyole kusaidiana na kuutoa mwili huo
Hospitalini hapo kwa lengo la kufanya taratibu nyingine
.
Aidha majirani hao
waliamua kuchukua mwili huo hadi nyumbani kwa Mwalukoba ambapo waliuweka kwenye
kiti ndani ya nyumba yake huku wakiendelea kumsubiri mwalukoba arudi
aliko ambapo baadaye alirudi nyumbani hapo akisindikiazwa na Mdogo
wake aliyefahamika kwa jina Gabriel Mwalukoba hadi nyumbani
hapo.
Kitendo hicho cha
kurejea kwa mwanaume huyo kilifanya mwenyekiti wa mtaa huo Ndugu Emanuel
Mwasibata kuhoji juu ya kutoweka kwa nyumbani kwakwe kwa muda wa
siku mbili huku kukiwa hakuna mawasiliano
yoyote.
Baada ya
kikao cha muda mrefu kati ya pande zote mbili mwanaume huyo alikubali kuupokea
mwili huo na hivyo kuanza kufanya taratibu za mazishi ambapo mazishi hayo
yalifanyika katika makaburi ya Iyela mida saa 12 jioni na kuhudhuriwa na familia
zote mbili pamoja na majirani wengine kutoka Uyole na Mama
John.
NA MBEYA YETU
Post a Comment