Binafsi nilikuwa na wasi wasi kuhusu ujana wangu na hasa changamoto kuwa maisha ya sasa ni fedha. Hofu yangu ilikuwa ni lini nitaanza kukamata fedha nyingi ili zisaidie mawazo na fikra zangu kufikia mahala ninapotaka.
Lakini, kutokana na kupanda kwa gharama na mkopo niliyochukua Serikalini kwa ajili ya masomo, niliamua kuendelea kuwatumikia mabwana wawili; chuo na kampuni ya sheria.
Nilijitahidi kadiri nilivyoweza kundunduliza sehemu ya kipato changu . Hatimaye nilifanikiwa kuwa na chumba. Nilinunua suti zangu tatu na pia jozi moja ya viatu.
Hata hivyo, wakati nanunua viatu sikuwa makini, kwani vilionekana vidogo; vilivyonibana na kunifanya nionekane mshamba. Siku niliyopiga ripoti ofisini, kila mmoja aliniangalia.
Ingawa sikujua ni kwa nini, lakini nilihisi walifanya hivyo kutokana na viatu vyangu!"- Barack Obama
Post a Comment