Jambazi
Sugu afariki katika majibishano ya silaha na polisi katika tukio
tofauti la kujibishana risasi na askari wa jeshi la polisi baada ya
kumfyatulia askari risasi na kumkosa huko maeneo ya Sokon 1 jijini hapa
jana majira ya jioni.
Kwa
mujibu wa kamanda wa polisi mkoani hapa Kamishna msaidizi wa polisi
Liberatus Sabas alisema kuwa mnamo majira ya saa11;15 huko mtaa wa
Onjaftian jeshi hilo lilifanikiwa kumuuwa baada ya majibishano ya risasi
na askari wa jeshi hilo jambazi sugu aliyefahamika kwa jina la Lembris
Taiko au kwa majina mengine doctor mbushii,general mwarusha, mwenye umri
wa miaka32-35 mkazi wa sokon 1 jijini hapa.
Kamanda
alisema kuwa awali walipata taarifa kwa wasamaria wema kuwa kuna watu3
wanaosadikiwa majambazi na kufuatilia maeneo ya tukio na kuizingira
nyumba walipojaribu kuingia ndani na kuwataka watu wote kujisalimisha
ghafla risasi zilianza kutoka ndani kupitia ukutani na kumkosa askari
hali iliyowalazimu askari kujibu mapigo na kufanikiwa kumuua jambazi
huyo.
Sabas
alisema kuwa uchunguzi uliofanya na askari wa jeshi hilo umebaini kuwa
ni jambazi sugu huyo alikuwa akitafuta na jeshi hilo na akishiriki
kwenye matukio ya ujambazi maeneo mbali mbali ikiwemo Arusha,Kilimanjaro
na Dar es salaam na alikutwa akiwa na bastola mmoja,aina ya bereta
iliyofutwa namba risasi moja chemba,ganda moja la risasi
iliyofyatuliwa,risasi 3za bunduki aina ya shortgun,na funguo mbali mbali
26 na mordem ya kampuni ya Airtel.
“Jambazi
huyu alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu na jeshi letu kwa kushiriki
kwenye matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha za moto tukio ambalo
lilitokea288\2012 huko maeneo ya olasiti jijini hapa ambapo walipora
bastola yenye no.T0620-11J00491 aina ya tisas”alisema kamada sabas.
Katika
tukio lingine jambazi huyo alijeruhiwa mguuni akafaniwa kutoroka lakini
jeshi la polisi lilifanikiwa kumua jambazi aliefahamika kwa jina la
peter Toshi katika majibizano hayo jambazi huyo alikutwa na bastola aina
tisas inayoaminiwa kuwa ndio ilioporwa ikiwa imefutwa namba zake.
Kamanda
sabas alisema kuwa kutoka eneo la tukio anabainisha kuwa mmiliki wa
nyumba aliokuwa jambazi huyo anaefahamika kwa jina moja la Swalehe au
baba Amiri ambaye hakuwepo wakati wa tukio hili jitihada za kumtafuta
zinafanyika ili aweza kuhojiwa juu ya uhusiano wao na jambazi aliyeuwa
na wapangaji wengine kwenye nyumba hiyo kutoa ushirikiano kwa jeshi la
polisi.
Hata
hivyo mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya mkoa ya mount
meru kwa uchunguzi zaidi na juhudi za kuasaka majmbazi wengine badao
zinaendelea kufanyika.
Post a Comment