Waziri
Mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai amezindua kampeni yake siku ya
Jumapili, huku akilalamika kuwa hakuna mageuzi yaliyofanyika kuhakikisha
uchaguzi wa Julai 31 unakuwa huru na wa haki.
Wazimbabwe
watapiga kura katika muda wa chini ya wiki tatu, kuhitimisha serikali
ya umoja kati ya Mugabe na Tsvangirai, ambao walilazimishwa kugawana
madaraka baada ya machafuko yaliyofuatia uchaguzi wa mwaka 2008.
Tsvangirai
alipata kura nyingi katika duru ya kwanza, lakini alijiondoa katika
duru ya pili kutokana na wafuasi wake kufanyiwa vurugu na vyombo vya
dola.
Rais
Mugabe ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 33, alizindua kampeni yake
Ijumaa iliyopita na kuwaambia wafuasi wa chama chake kuhakikisha ushindi
wa kishindo
Post a Comment