Na Kambi
Mbwana, Dar es Salaam
NI
Jumamosi nyingine msomaji wangu tunakutana tena katika safu hii, kwa ajili ya
kujadili mambo mbalimbali yanayohusu uhusiano na maisha yetu ya kila siku.
Hatua
ya muonekano wa picha hii inakuja kama kila mmoja ameamua kwa ridhaa
yake pamoja na kujiridhisha kuwa hapo ndipo mahali sahihi.
Hiyo ni
kwa sababu jambo hili linawagusa watu wengi katika jamii, hivyo kwa kulijadili
tunaweza kupeana hili na lile kwa ajili ya kuishi maisha ya furaha.
Wapo
wanaojichanganya na kuishi kwa presha katika mitaa yao, hasa pale wanaposhindwa
kuwa makini katika uamuzi unaohusu mambo ya mapenzi.
Msomaji
wangu mpendwa, katika jamii wapo baadhi ya kina dada wanaojirahisi wanapowaona
wanaume ambao ni machaguo yao halisi.
Wale ambao
kwa kawaida wanawapenda na kuwahitaji, ingawa wanashindwa kuwapa ukweli katika
kipindi cha mwanzo cha uhusiano wao huo.
Wanaanza
kujichekesha kwao. Hujilainisha kwa kila aina, huku wakishindwa kubaini hisia
zao na za wale wanaowapenda. Ndugu yangu, kumtamkia mwanaume au kuonyesha
upendo wake kwake, ni jambo moja na kujirahisisha pia ni jambo jingine.
Wewe kama
mwanamke, elewa unatakiwa uheshimu hisia zako kwa kujua vipi unaweza kufikisha
ujumbe au kumweleza mwanaume, lakini tu, asifikirie vingine.
Nasema
hivyo kwa sababu, kujichekesha ovyo ukiamini utafikisha ujumbe wako huko ni
kujidanganya. Wapo ambao watakuona kituko.
Watakuona
kicheche usiyejiheshimu kwa watu, hivyo sidhani kama utapendwa na kuthaminiwa.
Huo ndio ukweli na tunapaswa kuwa makini katika hili.
Wakati
ukijirahisi au kujilainisha kwa mwanaume, wenzako wanaweza kuchukua nafasi yako
kwa kuwa na msimamo wao, kuwa na maadili mema kwenye jamii.
Lazima
hilo tulijue kama tunahitaji kuwa na watu tunaowahitaji kuwa nao, ila si kwa
kuona kujipitisha kwake, kujichanganya naye hata pasipohitaji ni njia ya
kutamkiwa unapendwa na wanaume, maana huenda ukaonekana muhuni.
Hilo
tuliseme hadharani ili kila mtu ajue makosa yake yanayoweza kumgharimu katika
kipindi cha maisha yake, ukizingatia wapo mabinti ambao ni wasumbufu.
Kwa bahati
mbaya, usumbufu huo hauna faida kwao hasa pale wanapojikuta wanamsumbukia mtu
ambaye huenda hana muda wa kusikiliza kilio chake na kuambulia matusi.
Wanajikuta
wakinyanyasika kwa namna moja ama nyingine, hasa kwa kutoonyeshwa mapenzi ya
dhati, maana walifanya yale yasiyoruhusiwa.
Si wote ambao
wanapenda wanawake waliojipitisha kwao na kuweza kuishi nao vizuri. Hata kama
wakiwa pamoja, lakini kuna siku itatokea kashfa wanapoingia kwenye migogoro.
Mtu
anaweza kuona msichana huyo ni mrahisi, akamtaka mwenyewe, hivyo hawezi kuweka
akili yake kupoteza muda wa kumuwaza au kumlaki.
Kama
mwanzo hajaonyesha udhaifu wakati wa kuanzana na mpenzi wake, matusi, kejeli
hayawezi kuchukua nafasi, maana atakumbuka alivyopata tabu kwa ajili yako.
Sikatai
hata mwanamke anaweza kufikisha ujumbe wa mapenzi kwa mwanaume, lakini si kama
hivyo kwa kujipitisha pitisha ovyo, kutotumia nafasi nzuri kufikisha ujumbe wa
mapenzi.
Wakati
mwingine msimamo nao unahitajika na lazima uonyeshe kuwa wewe ni msichana
makini. Nayasema haya kwa sababu moja tu, wengi wanaumia kwa kuwapenda wanaume.
Wanawapenda
na kuwahitaji sana. Tatizo watafikisha vipi ujumbe wao kwa watu hao? Katika
kuumia huko, wameamua wajitoe mhanga, ila si kwa njia nzuri.
Kuna mengi
ya kufanya katika kufikisha ujumbe kwa mwanaume, hasa kwa wasichana wanaoumia
kwa namna moja ama nyingine, ila tutayajadili kadiri tutakavyopata nafasi hiyo.
Nakutakia
Jumamosi njema na tuendelee kuwa pamoja wiki ijayo katika ukurasa huu.
Tukutane
wiki ijayo.
0712
053949
0753
806087
Mwisho
Ongeza umakini
SWALI: Habari za leo Aunt Jeni? Mimi ni mvulana mwenye umri
wa miaka 25, tumekuwa tukikorofishana na mpenzi wangu mara nyingi, jambo la
kushangaza kila tunapogombana huniambia hanipendi, tena husema kuwa
ananitafutia sababu kubwa tuachane, kweli hapo kuna mapenzi ya kweli?
JIBU: Pole kwa yanayokukuta, kugombana ni mambo ya kawaida
katika maisha ya mahusiano, lakini kama anaendelea kusema atakutafutia sababu
ya kukuacha, inaonyesha wazi amedhamiria katika suala hilo, fungua macho na ongeza
umakini wa hali ya juu na umchunguze, lazima utapata sababu inayosababisha yeye
kusema hivyo.
SWALI: Habari yako Aunt? Matumaini yangu hujambo, kuna
umuhimu gani wa kuwa na mpenzi ambaye hakupendi wala kukujali, ila anahitaji
umtimizie kila kitu?
JIBU: Nashukuru mimi ni mzima, hapo hakuna mapenzi ya dhati,
anachokihitaji kutoka kwako ni kukutumia na kuondoka, mapenzi ya kweli huonekana
mapema.
Imeandaliwa na Jennifer Ullembo
Maoni 0655 747403
Post a Comment