|
Waziri
Mkuu Mstaafu Edward Lowassa akiwa ameambatana na makada wa chama,
wafanyabiashara wakubwa na viongozi wa wamachinga wa jijini Mwanza,
wakitembea kuelekea eneo la Makoroboi kwaajili ya mkutano wa muda mfupi
ambapo kiongozi huyo ambaye ni mbunge wa Monduli alikutana na wamachinga
wa jijini hapa. |
|
Alipowasili alikaribishwa kishupavu na vijana. |
|
Kisha akapanda mti eneo hilo ikiwa ni ishara ya kuthamini mazingira. |
|
Naye diwani wa Nyamagana Bhiku Kotecha alifungua mkutano huo kwa maneno machache. |
|
Wananchi kusanyikoni. |
|
Risala ya wamachinga ikisomwa. |
|
Wananchi wakitafakari wanayoelezwa. |
|
Wadau wakisikiliza kwa makini shughuli zinazoendelea mtaa maarufu wa wafanyabiashara ndogondogo hapa jijini Mwanza. |
|
Jiografia ya eneo la Makoroboi jijini Mwanza na umati wake. |
|
Mhe.
Lowassa akisalimiana na mmoja kati ya wachezaji wadogo kuliko wote wa
timu ya Machinga Fc inayoshiriki ligi ya kuwania kombe la Meya's Cup
jijini Mwanza. |
|
Timu ya Machinga inayoshiriki ligi ya Meya's Cup nayo ilitambulishwa. |
|
Lowassa akiwapa somo wamachinga Mwanza.
|
WAZIRI Mkuu mstaafu Bw.Edward
Lowassa amewataka wafanyabiashara wa Jiji na Mkoa wa Mwanza kuwawezesha
wafanyabiashara wadogo maarufu kwa MACHINGA ili kuwawezesha kupata mitaji ya
kujikwamua kiuchumi.
Akizungumza na Machinga wa shirika
la SHIUMA kwenye eneo la Makoroboi Jijini Mwanza leo mchana Mhe. Lowassa
ambaye ni Mjumbe wa NEC Wilaya ya
Monduli na Mbunge wa Jimboni humo alisema njia pekee ya kuwawezesha wamachinga
hao ni kuwachangia fedha ili kuwawezesha kujiendeleza kupitia biashara zao na
kuwapatia maeneo maalumu ya kufanyia shughuli zao.
|
Maneno yaliyowagusa. |
“Ninyi ni watanzania wenye kujiamini
na kujitafutia ridhiki kwa kufanya biashara zenu kwewnye Taifa lenu mkiwa huru
na amani, lakini mkiwa hamna mijati hamtaweza kufika pahali popote hivyo
niwaombeni sana wafanyabiashara wa Jiji na Mkoa wa Mwanza kuwachangia ili
kuwawezesha kupata mtaji wa kuwaendeleza
na kujiingizia kipato katika biashara zenu za ujasiliamali”alisema.
|
Makoroboi jijini Mwanza. |
Mjumbe huyo wa NEC alisema
kwamba Ilani ya CCM inatambua na inaelekeza kwamba vijana wataandaliwa na
kuanzisha vikundi vya ujasiliamali (SACOS) na kusajiliwa ili kuwapatia fedha
ikiwa ni mitaji ya kuwawezesha kujiendesha jambo ambalo ni utekelezaji wa Ilani
ya CCM ukurasa wa 88 na 89 hivyo tunataitekeleza kwa vitendo kama ambavyo ninyi
tayari mmeanza kuitikia na hilo ndilo limenileta hapa leo nikiwa kiongozi
ndani ya CCM.
“Nitaka nirudie msimamo wangu
kwenu kwani kuna baadhi ya vyombo vya habari vinaniandika kwamba nimekuja na
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Taifa Bw. Mwiguru Mchemba (Mbunge wa Jimbo la Iramba)kuvunja
ngome ya Chama furani hapa maeneo ya Jiji la Mwanza siyo kweli mimi niko na
marafiki zangu nimekuja kutokana na wito wenu ili kuwasikiliza sasa puuzeni
hayo”alisema.
|
Mhe.
Lowassa akimkabidhi hundi ya shilingi milioni 20 Bw.Matondo ambaye ni
mwenyekiti wa Shirika la Umoja wa wafanyabiashara wadogowadogo wa jijini
Mwanza (SHIUMA) huku akishuhudiwa na diwani wa kata ya Nyamagana Bhiku
Kotecha (anayepiga makofi). |
Bw. Lowassa alisema kwamba
kutokana na marafiki zake ambao aliwataja Bw.Christopher Mwita Gachuma (MNEC-
Tarime), Bw.Mathias Manga (MNEC-Arumeru), Bw.Raphael Chegeni (MNEC-Busega)
Bw.Shanif Hiran Mansoor(Mbunge-Kwimba) na Bw.Altaf Mansoor (Mkurugenzi wa MOIL)
ambao waliniomba na kunisisitiza kuwaona na kuwasikiliza nami nimewapa
utaratibu wa kuandaa Harambee kubwa ya kuwachangia na marafiki zangu wengine.
“Leo hii siyo harambee bali
nataka kuwachangia kianzio katika mfuko wenu na siku zote CCM inasema kwamba ni
lazima kuwapatia mtaji vijana hivyo nawapatia Cheki ya milioni 10 na jioni
ntwapatia shilingi milioni 10 jumla zitakuwa shilingi milioni 20 za kuanzia ili
kujipanga na harambee kubwa
|
Mmoja
kati ya wanakamati wa SHIUMA akionyesha hundi ya shilingi milioni 20
waliyokabidhiwa na Mhe. Lowassa kama sehemu ya harakati ya kutatua
masuala mbalimbali ya changamoto zao walizoziainisha kwenye risala. |
|
Mkutano huo wa
muda mfupi ulipo malizika tu Mhe. lowassa akiwa ameambatana na
wamachinga mguu kwa mguu walimsindikiza hadi hoteli aliyofikia.
CREDIT: GSENGO |
on Saturday, July 6, 2013
Post a Comment