Akaulizwa
nahodha mali hii ya nani?.Akasema ni mali ya Muhammed bin
Habiib.Akaambiwa mtu huyu tunamtafuta siku zote,anakaa Tabora sehemu
moja inaitwa Ndono kwa Mwanakurwa.
Akaulizwa
hii ni mizigo gani?.Akajibu hii ni tende.Akawaambia fungueni masanduku
muangalie.Kufunguliwa wakakuta madebe mengine yana baruti na mengine
yana risasi chini.
Akakamatwa
Yule nahodha akaambiwa sisi hatukupi nafasi yoyote.Akasema sawa lakini
mimi nimeajiriwa tu.Mtu akikodi nipelekee mzigo wangu huu pahala
Fulani,utajuaje ndani mna nini.Akaulizwa sasa utatufanzia taratibu
tuweze kumpata mtu huyo?.Nahodha akajibu mtu huyu nimemuwacha Unguja.
Akaambiwa tutakupa waranti wa
kumkamata.Akapewa waranti kwenda kumkamata Unguja.Alipofika sehemu moja
inaitwa Kichwele pana wadokozi wakaivuta kwenye mfuko wakidhani ni
pesa.Nahodha hakushtuka kuwa kilichovutwa ni waranti mpaka alipofika
Unguja.
Akaja
mpaka Unguja.Alipofika Darajani yeye anaingia na marehemu baba anatoka
Darajani.Wakasalimiana.Assalaam alaykum akajibu alaykum salaam.Aah
nahodha!.Akamwambia hapa ulipo siwezi kukuwachia hata dakika
moja.Umehatarisha maisha yangu.Umenambia ni mzigo wa tende kumbe baruti
na risasi.Mimi nimekamatwa.Waranti huu hapa!.Akatia mkono
mfuk
oni.Kutazama wapi! Waranti hana.
Ikawa watu wote pale wakawazingira.Kumwachia hataki.Watu wakamwambia ikiwa waranti huna rudi Darisalaama ukauchukue basi.Huyu muwache hapa hapa.Ukija na waranti tutakupa mtu wako.Yule nahodha akasema InshaAllah.
Baba
akawaambia wale watu "Nyinyi mukumbuke kuwa serikali ya kiiengereza
itaninyonga mimi.Akawaambia nipeni nafasi,wakamwachia.Akaenda mpaka
sehemu moja panaitwa Chukwani akapata ngarawa ikamchukua mpka sehemu
moja Dari salama panaitwa Tungi maeneo ya Kigamboni.
Alipofika
kule usiku.Pana mwarabu mmoja aitwa Saleh bin Suleiman katika
nduguze.Jee namna gani kaka?.Akamwambia tafadhali kaka tafuta pa kwenda
haraka.Hapa imekuja simu kuwa umeonekana Unguja ndipo hawa jamaa
wakaondoka.
Sasa
nifanze elimu gani.Akamwambia hapana elimu wala njia.Tukikwambia urudi
Mascat haiwezekani.Hatuna njia ya kukupeleka.Baba akasema mimi
nitakwenda Tabora.Utakwenda na nini?.Akasema Mungu atanipeleka.
Akatoka
akaja mpaka Morogoro,ana duka lake kaliweka.Akamkuta Hakim akamuuliz
vipi?.Hakim akamwambia imekuja habari kuwa umeonekana Unguja na
umekwishakamatwa ndipo askari wakaondoka lakini hawakutubakisha na
chochote.
Swali:Walichukua vitu dukani?.
Jibu:Walichukua vitu vyote.
Akamuuliza
sasa tutafanzaje?.Akamwambia hakuna njia.Mimi nakwenda
Tabora.Akamwambia lakini na Tabora ni mbali Muhammed.Akasema Mungu
atanisaidia.Basi kutoka Darisalaam mpaka kufika Tabora alikwenda kwa siku 21.
Swali:Kwa miguu?.
Jibu:Allaahu a'alam matumizi aliyotumia lakini inajulikana ni siku 21 kwa miguu.
Post a Comment