mkuu wa wilaya ya kilolo Gerald Guninita |
.....................................................................................................
Wakati wowote kuanzia kesho chama cha wafanyakazi mkoa wa Iringa kinategemea kutoa tamko dhidi ya mkuu wa wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Bw Gerald Guninita anayedaiwa kumkamata na kumweka mahabusu afisa usafiri wa wilaya ya Kilolo .
Taarifa ambazo mtandao huu wa ambazo umezipata zinadai kuwa viongozi wa chama cha wafanyakazi kesho mapema asubuhi kukutana na wanahabari na kutoa tamko kali dhidi ya mkuu huyo wa wilaya ya Kilolo.
Mtandao huu umepata kumtafuta mkuu huyo wa wilaya kwa njia ya simu japo amedai kuwa si kila kitu ni habari hivyo mtandao unasubiri kupata habari toka kwa viongozi hao wa wafanyakazi ili kujua undani wa sakata hili ambalo kisa cha viongozi hao kutoa tamko ni baada ya mkuu wa wilaya kudaiwa kumkamata na kumweka mahabusu afisa wa usafirishaji wilaya ya Kilolo kwa kile alichodai kuwa ameshindwa kutoa usafiri wa kuwapeleka askari wa kumlinda nyumbani kwake .
Credits: www.francisgodwin.blogspot.com
Post a Comment