Mkurugenzi Mkuu wa Airtel
Bwana Sunil Colaso akiongea wakati wa kufunga michuano ya Fainali ya mashindano
ya Airtel Rising Stars katika viwanja vya karume jijini Dar es
saalam.
Naibu Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makala akiongea wakati wa kufunga michuano ya
Fainali ya mashindano ya Airtel Rising Stars katika viwanja vya karume jijini
Dar es saalam.
Naibu Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Amos, akifatiwa na Raisi wa TFF sir Leodgar Tenga
pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso wakikangua timu kabla ya
kucheza mechi ya finali katika michuano ya Airtel Rising Stars , mechi ilikuwa
kati ya Morogoro na Mwanza.
Naibu Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Amos akiongea na wachezaji kabla ya kuanza mechi za
fainali.
Mlinzi wa Mwanza Ally Mnasi
(kushoto) akipambana na Evance Robert wa Morogoro wakati wa fainali kwenye
uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar mwishoni mwa wiki. Mwanza walishinda
1-0.
Naibu Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makala akikabidhi kombe la ubingwa wa Airtel
Rising Stars kwa nahaodha wa timu ya Mwanza Kelvin Faru kwenye uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume jijini Dar mwishoni mwa wiki.
Rais wa TFF Leodegar Tenga
akimvisha medali kocha wa timu ya taifa ya vijana Jacob Michaelsin kutambua
mchango wake kwenye mashndano ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa
yaliyomalizika uwanja wa Karume mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi wa Masoko wa
Airtel Tanzania Levi Nyakundi akikabidhi mfano wa hundi kwa mchezaji bora wa
Airtel Rising Stars Anna Hebron kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki.
Timu ya Mwanza wavulana imeibuka kidedea katika michuano ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars baada ya kuifunga Morogoro 1-0 katika mechi ya fainali iliyofanyika kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Nayo timu ya Kinondoni wametwaa taji la wasichana kwa kuifunga Ilala 1-0.
Timu ya Mwanza wavulana imeibuka kidedea katika michuano ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars baada ya kuifunga Morogoro 1-0 katika mechi ya fainali iliyofanyika kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Nayo timu ya Kinondoni wametwaa taji la wasichana kwa kuifunga Ilala 1-0.
Goli pekee la Mwanza
lilifungwa na mshambuliaji machachari Athanas Mdam kwa shuti kali katika dakika
ya 34. Mdam amejizolea sifa kem kem baada ya kuonyesha uwezo mkubwa wa kufunga
magoli na kutangazwa kuwa mfungani bora wa fainali hizo.
Mbali na Mdam, wachezaji
wengine waliong’aa katika mashindano hayo na kuchaguliwa na jopo la makocha ni
Arafat Mussa (mlinda mlango bora) kutoka Kinondoni na Omary Hussein (mchezaji
bora) kutoka Ilala.
Vile vile wachezaji sita
(wasichana watatu na wavulana watatu) wamechaguliwa kuiwakilisha Tanzania kwenye
kliniki ya kimataifa ya soka kwa vijana itakayofanyika Jamhuri ya Demokrasia ya
Kongo na kusimamiwa na makocha kutoka shule za mafunzo ya soka za Manchester
United. Wachezaji hao ni Anna Hebron, Niwael Halfan, Shelda Boniface, Athanas
Mdam, Thomas Chindeka na Omary Hassan.
Wakati huo huo Shirikisho
la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetaja majina ya timu za wavulana na wasichana
yakayofanyiwa mchujo ili kupata wachezaji 16 kutoka kila upande kwa ajili ya
kwenda kushiriki michuano ya kimataifa ya Airtel Rising Stars nchini Nigeria
mwezi Septamba.
Wachezaji hao kwa upende wa
wavulana ni Arafat Mussa, Fred Bakari, Emmanuel Innocent na Willy Karolo
(Kinondoni), Aziz Hassan, Omary Hussein, Joseph Mushi, Saddy Said na Said Danda
(Ilala), Rothan Mkanwa, Petro Mgaya, George Chota, Ramadhani Kondo na Optamus
Lupekenya (Morogoro), Bruno Shayo, Luseke Kiggi, Martini Lusseke na Athanas Mdam
(Mwanza), Thomas Chindeka, Miraji Kingaye na Salum Issa (Temeke) na Michael
Bosco (Mbeya).
Wasichana ni Najihati
Abbas, Stumai Abdallah, Anastazia Anthon, Tatu Iddi, Shelda Boniphace, Rehema
Yahya na Anna Bebron (Kinondoni), Niwael Halfan, Amina Ramadhan, Latifa Ahmed na
Alafa Abdul (Temeke), Vumilia Maharifa, Donisia Daniel, Maimuna Khamis na Amina
Ally Ilala), Khadija Hiza (Tanga), Mwamvita Tabago, Shakila Hashimu na Zainabu
Bakari (Kigoma), Shamimu Ally na Farida Mohamed (Ruvuma).
Akiongea wakati wa ufungaji
wa mashindano hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Sunil Colaso alisema
kuwa kliniki na mashindano ya Nigeria yatawapa fursa zaidi ya kujifunza na
kupata uzoefu na kusisitiza nia ya kampuni ya Airtel kuendeleza kudhamini
mashindano hayo.
Naye mgeni rasmi Naibu
Waziri wa Habari, Viajana, Utamaduni na Michezo Amos Makala aliwataka vijana
kuonyesha vipaji vyao na kuyataka makapuni mengine kujitokeza kudhamini michezo.
Wito wake uliungwa mkono wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF)
Leodegar Tenga.
Post a Comment