DAR ES SALAAM.
MWENYEKITI wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji
Joseph Warioba ametangaza tarehe rasmi ya kuanza kwa mikutano ya
Mabaraza ya Katiba ya wilaya, huku akiwaonya watu wa kada mbalimbali
vikiwemo vyama vya siasa kutokuingilia mikutano hiyo.
Vilevile Jaji Warioba alieleza sababu za Tume hiyo
kupendekeza Serikali tatu, huku akisisitiza kuwa suala hilo lilikuwepo
tangu siku nyingi na Tume iliamua kupendekeza Serikali tatu kwa kuwa
ndiyo ilikuwa njia pekee ya kuulinda muungano.
Kauli hiyo inaonekana kama kukijibu Chama Cha
Mapinduzi (CCM) ambacho kimependekeza kuwepo kwa Serikali mb
ili, ikiwa
ni siku chache baada ya kutolewa kwa Rasimu ya Katiba.
Mikutano hiyo inafanyika baada ya Juni 3 mwaka
huu, Tume hiyo kutoa rasimu ya Katiba na kusambaza katika vijiji, mitaa
na shehia kwa ajili ya kujadiliwa na wananchi, ambao nao watachangia
mawazo yao kwa wawakilishi wao waliowachagua kuwa wajumbe wa Mabaraza ya
Katiba ya Wilaya.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa jana, inaeleza
kuwa mikutano hiyo itaanza Julai 12 hadi Septemba 2 mwaka huu na
kutakuwa na jumla ya Mabaraza 177, Tanzania Bara 164 na Zanzibar 13.
Tayari Chama Cha Mapinduzi (CCM) kipo katika
mikakati kabambe ya kuhakikisha kuwa mapendekezo yake yanapitishwa huku
kikitumia wajumbe wa Mabaraza ya Katiba wakiwemo wa ngazi ya mtaa, huku
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye akiwaeleza
wajumbe wa mabaraza ya Katiba jijini Dar es Salaam juzi azma ya chama
hicho kuwa na rasimu mbadala.
Wakati CCM wakieleza hayo, Kamati Kuu ya Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) inakutana leo na kesho katika kikao
cha dharura jijini Dar es Salaam ili kujadili pamoja na mambo mengine
Rasimu ya Katiba Mpya.
Naye Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere,
anayemaliza muda wake, Profesa Issa Shivji, Juni 21 mwaka huu alisema
kama Rasimu ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano ikikubaliwa bila
mabadiliko makubwa itasababisha kuvunjika kwa Muungano.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Jaji
Warioba alisema hairuhusiwi kwa makundi, vyama vya siasa au mtu yeyote
kuingia katika mabaraza hayo kwa lengo la kushawishi kukubaliwa na maoni
ya aina fulani.
Alitoa ufafanuzi huo baada ya kuulizwa swali na gazeti hili, juu ya taarifa zilizopo kwamba baadhi ya vyama vya siasa nchini vimeandaa rasimu zao kwa lengo la kuwashawishi wajumbe wa mabaraza kupitisha maoni yao.
Alitoa ufafanuzi huo baada ya kuulizwa swali na gazeti hili, juu ya taarifa zilizopo kwamba baadhi ya vyama vya siasa nchini vimeandaa rasimu zao kwa lengo la kuwashawishi wajumbe wa mabaraza kupitisha maoni yao.
“Mikutano na Mabaraza ya Katiba siyo ya kupiga
kura bali ni kujadili na kutoa hoja ambazo zitakuwa na msingi kwa
masilahi ya taifa na siyo kutetea masilahi ya kundi au watu fulani,”
alisema Jaji Warioba na kuongeza;
“Hilo la vyama kuandaa rasimu zao kwa lengo la
kuingilia utaratibu huu sijalisikia, ila kikubwa ni kwamba si ruhusa
kuingilia mchakato huu kwa sababu utafanyika kwa mujibu wa taratibu
zilizopo,” alisema Warioba na kusisitiza; “Wananchi watoe maoni ambayo
yatasaidia kuiboresha rasimu iliyotolewa kwa kuweka mbele masilahi ya
taifa na kuepuka ubinafsi wa mtu mmojammoja au makundi ya aina yeyote.”
Alisema Tume yake itapokea maoni na mapendekezo
yote ambayo yatakuwa na lengo la kuiboresha rasimu ambayo itaweka umoja
wa kitaifa na siyo kuwagawa Watanzania.
CHANZO MWANANCHI.
Post a Comment