Ndugu zangu,
Muungano wa Nchi mbili ukizaa Serikali Mbili haujawa Muungano. Muungano wa Nchi MBILI huzaa nchi MOJA. Ukishindwa hilo, basi, utazaa nchi TATU.
Na hapo, Nchi Mbili zitakuwa zimeunda SHIRIKISHO au UMOJA fulani, ni kama EU. Mfano wa maji ya mto hautupi maana ya halisi na kwa uhalisia tulio nao. Maana, hata mito ikiungana, hatimaye hutengeneza mto mmoja. Mto Ruaha, Lukosi inapoungana hatimaye hupatikana mto Rufiji. Mto Rufiji hauingii bahari ya Hindi ukiwa na majina matatu.
Naam, mwanadamu havuki mto mara mbili. Ukishayakanyaga maji ya mto, basi, yamepita. Ukirudi njia hiyo utakuwa unavuka mto mwingine. Ndio maana Afrika mto mmoja huwa na majina tofauti.
NCHI NI KITU KINGINE. Nchi huwa na jina moja tu, mengine ni ya utani.
Ni Neno La Leo.
Maggid,
Iringa.
Post a Comment