Waziri
Mkuu Mizengo Pinda akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Banda la
Shirika la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya 37 ya Biashara ya
Kimataifa yaliyofikia tamati jana kwenye viwanja vya Mwl. Julius Nyerere
jijini Dar. Waziri Mkuu aliambatana na Waziri wa Viwanda na Biashara
Dk. Abdallah Kigoda pamoja na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini
Dk. Alberic Kacou.
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda ( wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa mmoja
wa Wajasiriamali wanaofadhiliwa na UNIDO kwenye banda la Shirika la
Umoja wa Mataifa akiwa ameambatana na Waziri wa Viwanda na Biashara Dk.
Abdallah Kigoda (kushoto) pamoja na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa
nchini Dk. Alberic Kacou (wa pili kulia) wakati wa sherehe za kufunga
Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa jijini kwenye viwanja vya
Mwalimu Julius Nyerere leo.
Tuzo
maalum waliyokabidhiwa shirika la Umoja wa Mataifa nchini kwa kutambua
mchango wao wa kuhamasisha Jamii (UN Special recognition for community
awareness) wakati wa sherehe za kufunga Maonesho ya 37 ya Biashara ya
Kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere.
Mratibu
Mkazi wa Umoja wa Mataifa Dk. Alberic Kacou akipokea Tuzo ya Ngozi
iliyotengenezwa kinyumbani kutoka kwa Wajasiriamali wanaodhaminiwa na
UNIDO wakati alipotembelea Banda la Shirika hilo leo kwenye maonyesho ya
37 ya Kimataifa ya Biashara yalifungwa rasmi jana na Waziri Mkuu Mh.
Mizengo Pinda.
Mkufunzu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam ( DIT) Marwa Wambura (kulia) akitoa
maelezo kwa Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic Kacou
ya malighafi za ngozi zinazotumika kutengeneza bidhaa mbalimbali na
wajasiamali wanaofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza
viwanda Duniani (UNIDO).
Mratibu
Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic Kacou akiwa kwenye picha
ya pamoja na wafanyakazi wa vitengo mbalimbali vya Ofisi za Umoja wa
Mataifa nchini. (UN-Tanzania Delivering as one).
Banda la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya Sabasaba likiwa limeandika ujumbe unaosema “Umoja wa Mataifa inafanya kazi kwa ajili yako-kuboresha maisha ya watoto, wakinamama na vijana”.
Mratibu
Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic Kacou alipotembelea banda
la Wizara ya Fedha wakiwa ni wadau washirika wa Maendeleo nchini.
Mratibu
Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic Kacou akibadilishana
mawazo na mmoja wa wadau alipotembelea banda la Wizara ya Fedha ikiwa ni
kudumisha ushirikiano na Serikali ya Tanzania.
Post a Comment