Vikosi vya
askari mgambo na askari polisi ambao ni wanafunzi wa chuo cha taaluma
ya Polisi Moshi wakishuka kutoka mlima Kilimanjaro ambako walikuwa
wakifanya shughuli za kuzima moto uliowaka jumapili ya
Julai
Mchakamchaka
Naibu waziri
wa maliasili na utalii Lazaro Nyarandu akiwasili katika viwanja vya
ofisi ya hifadhi ya taifa ya mlima Kilimanjaro KINAPA kuwapokea na
kuzungumza na asakari walioshiriki zoezi la kuzima moto mlima
Kilimanjaro.
Askari
walioshiriki zoezi la kuzima moto.
Kaimu
mkurunzi wa hifadhi za taifa Martin Loibook akizungumza wakati wa kuwapokea
asakri walioshiriki kuzima moto mlima Kilimanjaro.kushoto kwake ni
naibu waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nayarandu na katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro Issa
Faisal.
Askari
shujaa
Mhifadhi mkuu
wa hifadhi ya taifa ya mlima Kilimanjaro Erastus Lufunguro
akisoma taarifa mbele ya naibu waziri wa maliasili na utalii,Lazaro
Nyarandu.
Mhifadhi mkuu
wa hifadhi ya taifa ya mlima Kilimanjaro Erastus Lufunguro
akimkabidhi naibu waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyarandu
taarifa kuhusiana na moto uliokuwa ukiwaka mlima
Kilimanjaro.
Naibu waziri
wa maliasili na utalii Lazaro Nyarandu akizungumza na kundi la
askari walioshiriki zoezi la kuzima moto mlima Kilimanjaro
Naibu waziri
wa maliasili na utalii Lazaro Nyarandu akizungumza na kundi la
askari walioshiriki zoezi la kuzima moto mlima Kilimanjaro
Wakuu wa
vikosi vilivyoshiriki kuzima moto mlima Kilimanjaro.
Naibu waziri
wa maliasili na utalii Lazaro Nyarandu akiwapongeza askari
walioshiriki kuzima moto Mlima Kilimanjaro.
Naibu waziri
wa maliasili na utalii Lazaro Nyarandu akizungumza na wafanyakazi
wa hifadhi ya taifa ya mlima Kilimanjaro.
Naibu waziri
wa maliasili na utalii Lazaro Nyarandu akizungumza na viongozi wa
askari mgambo
Naibu waziri
wa maliasili na utalii Lazaro Nyarandu akizungumza na viongozi wa
askari mgambo ,kushoto kwake ni mhifadhi mkuu wa hifadhi ya taifa ya
mlima Kilimanjaro Erastus Lufunguro.
Picha zote na
Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi
******
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Moshi
SERIKALI imeyashukuru makundi mbalimbali pamoja na viongozi wa mkoa wa Kilimanjaro kufanikisha zoezi la kuzima moto katika hifadhi ya mlima Kilimanjaro ulioteketeza zaidi ya ekari 40 katika eneo la Amboni .
Naibu waziri wa maliasili na utamaduni Lazaro Nyarandu ametoa pongezi hizo leo wakati akiwapokea vikosi vya askari polisi wa chuo cha taaluma ya Polisi cha mjini Moshi pamoja na asakari mgambo walioshiriki zoezi hilo la kuzima moto.
Amesema serikali imefurahishwa na moyo wa kujitolea uliofanywa na makundi hayo ya askari pamoja na watu wengine kwani wameonesha moyo wa uzalendo wa kuijenga nchi yao na kwamba ushirikiano huo ndio unaohitajika ili kutokomeza majanga mengine yote yanyo tokea katika taifa. Amesema usalama na ubora na kuwepo kwa uhifadhi wa mlima Kilimanjaro utasaidia uchumi wa nchi pamoja na wapenda milima na mazingira duniani kuona uoto wa asili na theruji ya mlima huo vikiendelea kuwepo.
Awali akiwasilisha taarifa kuhusu kuzuka kwa moto huo Mhifadhi mkuu wa hifadhi ya mlima Kilimanjaro Erastus Lufunguro amesema KINAPA iliweka kambi tano maalum kwa ajili ya kuhudumia waliokuwa wakishiriki zoezi la kuzima moto.
Amesema moja ya kambi hizo ilikuwa eneo la Marangu kwa ajili ya kuhudumia eneo la Kilema juu ambapo zote kwa pamoja zilikuwa na askari mgambo 128 kutoka wilaya zote za mkoa wa Kilimanjaro sanjari na askari 54 waliopo mafunzoni katika chuo cha polisi CCP.
CREDIT: MICHUZI MATUKIO BLOG
Post a Comment