Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe na waziri
mkuu Morgan Tsvangirai Reuters |
Na Lizzy Anneth
Masinga
Waziri wa fedha nchini Zimbabwe amesema kuwa
bado zimbabwe haina fedha za kutosha kulipa gahrama za uchaguzi unaotarajiwa
kufanyika katika kipindi cha miezi mitatu.
Uchaguzi nchini Zimbabwe utafanyika tarehe 31
mwezi Julai huku Rais wa nchi huyi Robert Mugabe akitazamia kumshinda Waziri
Mkuu, Morgan Tsvangirai.
Baada ya maelfu ya Raia wa Zimbabwe kushindwa
kujiandikisha kwenye orodha ya wapigakura, Waziri wa Fedha Tendai Biti ameomba
Mamlaka zinazoshughulikia maswala ya uchaguzi kuongeza muda wa kujiandikisha
mpaka juma lijalo.
Biti ametoa wito kwa Viongozi wa Jumuia ya
Maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika (SADC) kuingilia kati kwa kuwa mabadiliko
katika maswala ya Usalama, Vyombo vya Habari na Tume ya uchaguzi bado
hayajafanyiwa kazi.
Biti amesema huu ni wakati wa SADC kutathimini
kama inawezekana kwa Zimbabwe kufanya uchaguzi ulio wa haki.
Biti ametoa shutma kwa Chama za ZANU-PF kuwa
kimeipa kandarasi Kampuni moja kutoka nchini Israel ili kurubuni uandikishaji wa
Wapigakura.
Via - kiswahili.rfi.fr
Via - kiswahili.rfi.fr
Post a Comment