Na
Esther Macha, Mbeya
MKULIMA
wa Kijiji cha Ikumbi Songwe wilaya ya Mbeya vijijini Nasibu Matinya (25)
ameuwawa kikatili kwa kupigwa mawe na mapanga ,fimbo kisha kuchomwa moto baada
ya kuiba mahindi debe tatu ,maharage bakuri 10.
Kwa
mujibu wa Kamanda wa polisi Mkoani Mbeya Diwani Athuman katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana alisema tukio hilo
limetokea Agosti 4 mwaka huu majira ya saa 18:40 huko Ikumbi Songwe wilaya ya
Mbeya vijijini.
Kamanda
Diwani alisema kuwa mkulima huyo aliuwawa
kwa kupigwa na kundi la wananchi walioamua kujichukulia sheria mkononi
kwa kutumia mapanga, mawe na fimbo kisha kumchoma moto.
“Marehemu
baada ya kupata kipigo hicho wananchi hao waliamua kumchoma moto mpaka kubaki
majivu”alisema.
Aidha
Kamanda huyo alisema kuwa chanzo cha
kuuwawa kwa marehemu ni wizi baada ya marehemu kuiba mahindi debe 3
maharage bakuri 10, doti 3 za vitenge na pampu ya baiskeli 1 nyumbani kwa
jirani yake Hebron mwakimonya.
Hata
hivyo kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishana msaidizi wa polisi Diwani
Athumani ametoa wito kwa jamii kuacha mara moja tabia ya kujichhukulia sheria
mkononi na badala yake kuwafikisha watuhumiwa wanaowakamata katika mamlaka
husika ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.
Akizungumzia
kuhusu watu waliokamatwa Kamanda Diwani alisema hakuna mtu yeyote aliyekamatwa
kuhusiana na tukio na jeshi la polisi bado linaendelea na uchunguzi ili kuweza
kuwabaini watu waliofanya hivyo.
“Baada
ya kufanya unyama huo kundi hilo la wananchi lilikimbia baada ya kuhakikisha
kuwa marehemu ameteketea mwili wote.
Post a Comment