Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa na Mkurugenzi wa
Shughuli za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dar es salaam Shumbana
Taufiq kabla ya kuanza ziara yake katika Taasisi za SMZ zilizopo Mjini
Dar es salaam. Kulia yao ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Issa Mlingoti.
Balozi
Seif akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha ZBC Dar Msangu Said
Mohammed alipotembelea chumbna cha Habari cha Kitengo hicho. Kushoto
ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo
Issa Mlingoti na Kushoto yake ni Mkurugenzi Mkuu wa ZBC Hassan Mitawi.
*****************************************
Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar itajitahidi kuona changamoto zinazowakabili
watendaji wa Ofisi ya Uratibu wa shughuli za Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar waliopo Dar es salaam zinashughulikiwa vyema kwa kupatiwa
ufumbuzi ili kuleta ufanisi katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPO CHINI
Kauli
hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi alipofanya ziara maalum ya kuangalia shughuli za kazi za watendaji
wa Taasisi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizopo Dar es salaam
akianzia na Ofisi ya Uratibu wa shughuli za Serikali.
Ofisi
hiyo iliyopewa mamlaka ya kuratibu uwajibikaji wa Taasisi zote za SMZ
zilizopo Mjini Dar es salaam itakuwa chini ya Ofisi Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar kufuatia mabadiliko yaliyofanywa na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Sheni katika baadhi
ya Taasisi za Serikali siku moja iliyopita.
Balozi
Seif alisema Serikali iliamua kwa makusudi kuanzisha Ofisi hiyo mnamo
mwaka 1986 kwa lengo la kuwa kiunganishi cha upatikanaji wa huduma za
kiuchumi kiurahisi kati ya Zanzibar na Tanzania Bara sambamba na
mashirika pamoja na Taasisi za Kimataifa.
Katika mbinu
za kujaribu kupunguza matumizi ya uendeshaji wa Ofisi Balozi Seif
alifahamisha kwamba Serikali ina nia ya kulipata jengo hilo kwa
kuwasiliana na Serikali ya Muungano hata kwa njia ya kubadilishana {
Butter system } jambo ambalo gharama zinazotumika hivi sasa zinaweza
kusaidia masuala mengine.
Akizungumzia
Kitengo cha Habari kilichojumuisha Magazeti ya Serika { Zanzibar Leo },
shirika la Utangazaji Zanzibar { ZBC } na Habari Maelezo Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza wana Habari hao kwa umahiri wao wa
kufanya kazi licha ya kuzunguukwa na mazingira magumu ya kikazi likiwemo
tatizo la usafiri .
Aliuagiza
Uongozi wa Taasisi hizo kufanya utaratibu wa kuandika mapendekezo ya
vile vifaa muhimu zaidi vya mwanzo na kuyawasilisha Serikalini ili
kuangalia namna ya kusaidia uwezeshaji.
Balozi
Seif alisema kutokana na mabadiliko ya haraka na ya kila wakati katika
sekta ya Habari, watendaji wake wanalazimika nao muda wote waende na
wakati.
“
Kwa vile Serikali Kuu tumeshaamua Sekta zetu za Habari zijiendeshe
kibiashara. Sasa Baraza letu la Wawakilishi kuanzia mwezi Oktoba katika
vikao vijavyo litalazimika kulipa matangazo ya moja kwa moja ya vituo
vya Habari vya ZBC Redio na Tv “. Alisisitiza Balozi Seif.
Aliuagiza
Uongozi wa Sekta ya Habari kufanya utafiti utakaofahamu tatizo
linalosababisha matangazo ya ZBC Redio na Televisheni kutopatikana
katika maeneo ya Tanzania Bara.
“Mimi
nilikuwa msikilizaji mkubwa wa Vipindi vya Redio hasa kile cha kutoka
magazetini hakinipiti ninapokuwa Dar pamoja na matangazo ya ZBC TV. Hata
nikiwa Dodoma Matangazo ya Redio nilikuwa nikiyapa lakini sasa yote
yamekatika siju kwa nini? “ Aliuliza Balozi Seif.
Mapema
Mkurugenzi wa Shughuli za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dar es
salaam Shumbana Taufiq alisema Taasisi hiyo ambayo ni kiunganishi muhimu
cha mawasiliano kati ya Zanzibar na Mashirika na Taasisi za Kimataifa
imekuwa na mazingira magumu ya utekelezaji wa majukumu yake kutokana na
tatizo la kutoingiziwa fedha kwa wakati.
Mkurugenzi
Shumbana alisema gharama za kupanda kwa maisha hasa katika Jiji la Dar
es salaam kumewafanya watendaji hao kuishi katika maisha ya kubahatisha
suala ambalo hupunguza ari na moyo wa uwajibikaji.
“
Wakati mwengine sisi wasimamizi tunakuwa katika hali ya unyonge wakati
hata zile fedha za pencheni kwa wafanyakazi wastaafu
zinachelewakutufikia na matokeo yake kuleta malalamiko kwa wazee wetu
hao waliopo hapa Dar “. Alifafanua Mkurugenzi Shumbana.
Nao
baadhi ya watendaji wa taasisi hizo wakiwemo viongozi wao wa Wizara na
Idara wamezitaja baadhi ya changa moto zinazokwaza utekelezaji wao wa
kazi ikiwa ni pamoja na ukosefu wa vifaa vya kazi, usafiri pamoja na
kuomba kuongezewa posho ili kukidhi mahitaji.
Awali Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar alizitembelea Ofisi ya Idara ya Uratibu,
Kitengo cha Utawala na Rasilmali Watu, uratibu wa misaada na Mipango
pamoja na ile ya wana Habari.
Post a Comment