DC RUGIMBANA |
SIKU chache baada ya Kamati iliyoundwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana kukabidhiwa tuhuma nzito zinazohusu Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana kuwafanyia unyama wananchi wa Mtaa wa Ukombozi Kata ya Kivule Dar es Salaam, uongozi wa chama hicho wilaya ya Ilala nao umejitosa kusaka ushahidi zaidi.
Kamati ya Kinana inayoundwa na vijana kutoka Dodoma hivi karibuni ilizungukia maeneo kadhaa ikiwamo Kivule kubaini mambo yanayokwamisha utekelezaji wa Ilani ya chama hicho kuelekea 2014, 2015.
Katika ziara hiyo, kamati hiyo ilikabidhiwa ushahidi wa CD zinazoonyesha jinsi nyumba za wananchi zaidi ya 300 zilivyovunjwa, mabaki ya maganda ya mabomu ya kutoa machozi yaliyorushwa na polisi kwa niaba ya Umoja wa Vijana wa Kikristo Tanzania (UVIKIUTA) Oktoba mwaka jana. Rugimbana na mdhamini wa Uvikiuta.

Licha ya ushahidi wa wananchi uliokabidhiwa kwa Kamati ya Kinana, viongozi wa chama hicho ngazi ya wilaya wanaonekana wakihaha kusaka ushahidi zaidi wa mgogoro huo kupitia kwa wakazi wa eneo hilo ambao ni wazawa kujua kiini na asili ya ardhi hiyo.
Katika juhudi hizo, uongozi wa CCM Wilaya ya Ilala wiki iliyopita ulipiga hodi Kivule na kufanya mazungumzo na wananchi na kukagua maeneo na vifusi kadhaa vya nyumba zilizovunjwa.
Katibu wa chama hicho Wilaya ya Ilala, Ernest Chale pamoja na ujumbe wake walijionea uharibifu mkubwa wa mali ambako walisikika wakisema wazi kwamba haki za binadamu katika eneo hilo zilivunjwa.
Uchunguzi uliofanywa na MTANZANIA umebaini kuwapo msuguano miongoni mwa viongozi wa CCM wilaya ya Ilala, ambao wanahoji UVIKIUTA yenye wanachama ambao hawafahamiki vema kuhodhi ardhi yenye ukubwa wa zaidi ya ekari 1000 katika Jiji la Dar es Salaam bila kuwa na nyaraka zinazoeleweka.
Habari zinasema CCM wanaona mgogoro huo kama hautamalizika mapema unaweza kuwa kikwazo kwao kwa kuwanyima kura katika uchaguzi ujao kuanzia ule wa Serikali za mitaa mwaka 2014 na uchaguzi mkuu 2015 hivyo kutoa nafasi ya mteremko kwa wapinzani.
Lakini upande mwingine wanautafsiri mgogoro huo kwamba umevuka mipaka kwa viongozi wa Serikali kutumia vibaya madaraka yao, jambo ambalo linakichafua chama machoni mwa wananchi
Post a Comment