Mhe. Edward Lowassa (Mb.)Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Monduli
akizungumza wakati wa kikao na Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa katika kupitia Taarifa ya Utekelezaji wa
Diplomasia ya Uchumi ya Wizara. Kikao hicho kilifanyika katika Ofisi
Ndogo za Bunge tarehe 19 Agosti, 2013.
Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, akiwasilisha Taarifa ya Wizara ya Utekelezaji wa Diplomasia
ya Uchumi mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge (hawapo pichani).
Baadhi ya Waheshimiwa wa Wabunge ambao pia ni Wajumbe wa Kamati ya
Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani).
Kikao kikiendelea.
Baadhi ya Wakurugenzi na Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa wakifuatilia kwa karibu taarifa iliyokuwa
ikiwasilishwa na Mhe. Membe (hayupo pichani).Picha na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Post a Comment