Ningependa
kwanza kwaombea wazee wetu walio tangulia kwenye haki waanzilishiwa
taifa letu TANZANIA MZEE J.K.NYERERE NA MZEE ABEID AMANI KARUME, Wazee
wetu hawa wakati wanaanzisha huu muung
ano walikiuwa na nia nzuri ukifatiria na hali ya siasa iliyo kuwepo wakati huo ,ni kweli kabisa upendo wa wazee hawa ulikuwa ni wa haina yake na mpaka walipofikia kuamua kitendo hicho walikuwa ni majasiri na mashujaa.
ano walikiuwa na nia nzuri ukifatiria na hali ya siasa iliyo kuwepo wakati huo ,ni kweli kabisa upendo wa wazee hawa ulikuwa ni wa haina yake na mpaka walipofikia kuamua kitendo hicho walikuwa ni majasiri na mashujaa.
Ni
kweli muungano umetuletea mambo mazuri mengi na kunamambo ambayo
ukiangalia kwa kirefu au kwa upana unaona kuna makosa ambayo yanaweza
kutatuliwa na watu wanaoipenda Tanzania (maana yake naposema hivi kuna
vibaraka wanaotumiwa na watu kutoka nchi za nje ili kuvunja muungano huu
hau kuigawanya nchi kwa makabira na kwa dini)
Wa
Tanzania kubomoa ni rahisi na kujenga siyo mchezo ndugu zangu tukumbuke
kitukimoja sisi kama waafrica tumetawailiwa na waarabu wariotoka makwao
tumetawaliwa na wazungu walio toka makwao na kutufanya watumwa na
kuuwa mababu zetu waliokuwa wakitembea maili na maili na kutufanya
sisi ni mbwa na leo hii hayo yote tuna aanza kuyasahau na kutaka kurudi
katika ukoloni wa mambo leo,
Ndugu zangu tukumbuke haya yote na damu za mababu zetu kutokea mwanza,kigoma,tabora,songea, tanga
manyema congo,na ungunja,pemba, na mikoa yote ya TANZANIA,Damu
iliyomwangika isije ikapoteabure tukumbuke tunapotoka ndio tupate katiba
yenye utaifa, ni mazuri ghani yaliyopo kwenye katiba ya zamani? na
mambo ghani ambayo hayafai kwenye katiba hiyo ya zamani,
je
mfumowa serikali mbili unafaa au vipi? au serikari tatu? au tuwe na
serikali moja tuu na nchi iwe na state maana yake itakuwa inaitwa UNITED
STATE OF TANZANIA and tuwe na Raisi ,makamu waRaisi na Waziri mkuu ?
ndugu
zangu kwanza hapa shida siyo serikari tatu au mbili au moja shida ni
moja tuu ambayo inarudisha maendeleo nyuma na kufanya asilmia karibu 65
ya waTanzania kubaki masikini na kuendelea kuwa masikini,Tatitizo ni
hili hapa ni Good governance, Responsibility.
Acountabilty, Deliverance and good economic policies.nakingine
ni hiki agenda ya Tanzania au Manifesto ya Tanzania iko wapi wakati wa
mwalimu ilikuwa ni ujamaa wa kujitegemea je sasa hivi nini?
kwa
upande wangu kutokana na nchi yetu kuwa bado ni maskini hatuwezi kuwa na
serikari tatu uendeshaji wake utakuwa ni wagharama na pila atuwezi kuwa
na maraisi watatu,maoni yangu yako very simple ningependa tuwe na
serikali moja tuu maana yangu mimi sijui kuna nchi inaitwa Tanganyika au
Zanzibar kitu nachojuwa ni kwamba nchiziliungana na kutengeneza au
kuzaa taifa linaloitwa Tanzania,
kwa maana yangu au kuelewa kwangu ni kwamba tunapashwa kuwa serikali moja ambayo itakuwa na Raisi na makamu wake na waziri mkuu,
baadala ya ya kuwa na mikoa tuwe na state na hizi state zitakuwa chini ya serikali ya katikati au central,
hizi
state zitakuwa na Katikiro natumia jina la kiafrika ambaye hatakuwa
anachaguliwa na wananchi na kazi zake ni kuwatumikia wananchi na
kuhakikisha hanatimiza mipango yote ya serikali kwa uhakika na bila
mchezo na muda wake wa kufanya kazi ni miaka kumi mitano,na mitano kama
hatachaguliwa na wananchi tena.
Raisi
hatachaguwa Governor ambaye kazi yake ni kuangalia mambo ya utendaji wa
sela za serikali yani sera za nchi siyo za chama na kazi ya usalama
yaani ataitwa Overseer na hii ndiyo itakuwa kazi yake tu na anaweza
kuongezewa majukumu mengine,
Jee
hizi state zitaendeshwa vipi zitakuwa zinakusanya mapato na asilimia 37
yawe yanabaki kwenye state na asilimia 63 yanaenda kwenye Central
government na tuwe na mawaziri wa kuitumikia nchi moja na na tuwe na
bunge moja tu lenye wabunge 250 wabunge 70 kutoka visiwani na wabunge
180 kutoka bara na tuwe na bunge la wezee au nyumba ya juu amabayo
itakuwa na wazee 50 tuu ambayo itakuwa na wawakilishi wa dini
waislam2,wakristu2,wahindu2, wazee wetu wa au wakuu wa chief2,nafasi
zilizi baki watachuguliwa na bunge na kuteuliwa na raisi yaani retired
jaji,police,wakuu wa majeshi,doctors,Raisi, mawaziri,na kiwango cha umri ni kuanzia miaka 60.
Pamaoja
na haya yoteniliyosema bado tutakuwa pale pale kama hatutaweza kuwa na
agenda au manifesto ya nchi siyo ya CCM,au CHADEMA ,au CAF,DP,auTLP ni
mengi ya kusema hapa lakini naona kwanza ni achihe hapo kwenye swala la
serikari moja,
Je
kuhusu serikali mbili ni vipi? Kama tutaendela kuwa na serikali mbili je
nini kinachotakiwa kufanywa sababu visiwani kunaonekana kwake mpaka
sasa inaonekana kama ni nchi ndani ya muungano iko na bendera,iko na
wimbo wa taifa, lakini bara hakuna wimbo wala bendera kw upande wangu
tungeweza kujifunza kwa wenzetu wa hapa uingereza wako na nchi nne ndani
ya muungano wa united kingdom, je nini ambacho tunacho weza kujifunza
kutoka kwao au tunaweza kijifunza nini kutoka kwa hawa jamaa wa united
emirates
Ndungu
zangu ningependa sana hoja hii tuichambuhe kwa makini na kwa kirefu
kutokana na historia yetu na tunapotoka sababu naamini Tanzania ya leo
iko na wasomi wengi na wenye vipaji naomba sana tufunguke tuwe wazi
tutoe maoni kwakirefu
Natanguliza shukrani kwa bwana Mchuzi na kwa waTanzania wote watako soma maoni yangu au kuchangia maoni yetu.
CHANZO http://michuzi-matukio.blogspot.com
Asanteni sana.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU IBARIKI AFRICA
Na Mdau Yussuf.
Post a Comment