Tindika ikiwa katika ndoo tayari kwa kuuzwa, uchunguzi umebaini kuwa bidhaa hii hatari huuzwa kiholela jijini Dar es Salaam.
Mfanyabiashara maarufu na Mmiliki wa maduka ya Home Shopping Center(HSC), Said Mohamed Saad, ameliwa kwa kumwagiwa tindikali.
Rais Jakaya Kikwete akimjulia hali Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Fadhili Soraga.
SIKU
chache baada ya wasichana wawili raia wa Uingereza kumwagiwa tindikali
mjini Zanzibar, imebainika kuwa, tindikali za aina mbalimbali zinauzwa
kiholela kama njugu jijini Dar es Salaam.
Uchunguzi
uliofanywa na gazeti hili unaonyesha kuwa jijini Dar es Salaam yapo
maduka mengi yanayouza tindikali ya kila aina na bidhaa hiyo inauzwa
bila ya udhibiti wowote kuanzia Kariakoo hadi Vingunguti.
Wiki
iliyopita, Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele alitoa miezi
mitatu kwa wafanyabiashara wa tindikali kujisajili ili kuzuia
kuongezeka kwa matukio ya uhalifu kwa kemikali hiyo nchini.
Uchunguzi
uliofanywa na gazeti hili katika mitaa ya Dar es Salaam, umebaini kuwa
tindikali za aina mbalimbali zinapatikana kwa wingi katika maduka ya
rejareja na jumla, huku wauzaji wa bidhaa hizo wakishindwa kutoa
tahadhari yoyote kwa wateja wao.
Imebainika
kuwa tindikali zinazopatikana kwa urahisi zaidi ni Sulphonic Acid
ambayo imetajwa kutumika kutengeneza sabuni za maji (multipurpose
detergents), Sulfuric acid inayotumika kutengeneza maji ya betri na
Hydrochroric acid inatumiwa na wajasiriamali kutengeneza dawa za usafi.
Kemikali
nyingine ambayo imeelezwa na watumiaji wake kuwa ni hatari ni Hydrogen
Peroxide ambayo hutumika kusafisha mafuta ya mawese yanayotumika
kutengenezea sabuni za kipande.
Katika
Mtaa wa Gerezani Kariakoo, kuna duka maalumu la kuuza kemikali
mbalimbali kwa bei ya rejareja na jumla, kemikali hizo zinauzwa kati ya
Sh4,000 hadi Sh6,000 kwa kilo moja kutokana na aina yake.
Muuza
kemikali mmoja katika mitaa ya Sinza wilayani Kinondoni, ambaye
hakutaka kutaja jina lake gazetini kuhofia usalama wake, alisema
biashara hiyo ilianza kushamili miaka mitatu iliyopita baada ya
kuanzishwa kwa mafunzo ya kutengeneza bidhaa mbalimbali zinazotumia
kemikali.
“Matangazo
yanayotolewa katika vyombo vya habari kuhusu ujasiriamali wa
kutengeneza sabuni aina mbalimbali, ndiyo yaliyochochea kuongezeka kwa
mahitaji ya tindikali hapa nchini.
Kwa mfano, (anamtaja mhusika) anafundisha namna ya kutengeneza maji ya
betri za magari kwa kutumia Sulphuric acid, unategemea wajasiriamali
wakanunue wapi hiyo tindikali?” anahoji.
Matukio ya kujeruhiwa na tindikali.
Agosti
7 mwaka huu raia wawili wa Uingereza, Kate Gee na Kirstie Trup wote
miaka 18 walishambuliwa kwa tindikali na watu wasiojulikana wakati
wakitembea kwenye mitaa ya Stone Town mjini Zanzibar. Raia hao
walisafirishwa na kurudishwa Uingereza ambako wanaendelea na matibabu.
Kabla
ya kuondoka nchini, Rais Jakaya Kikwete aliwatembelea raia hao
hospitali na kusema kuwa tukio hilo limeitia aibu nchi kwa mataifa ya
nje na kuliamuru Jeshi la Polisi kuhakikisha linawakamata na
kuwafungulia mashtaka wote waliohusika. MWANANCHI.
Post a Comment