Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

KUIGA IGA MAMBO "KWAMVUA NGUO" SAMWEL SITTA .... AIBIKA VIBAYA SANA

Photo: Sitta ajeruhiwa 

*Aanguka vibaya harambee ya kanisa Busega
*Magufuli, Membe na Mwekyembe wakwama

HARAKATI za Waziri wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta, kufanya kile ambacho kimekuwa kikifanywa na wanasiasa wa kariba yake ambao amekuwa akiwashambulia kwa kujihusisha na masuala ya kijamii, zimegonga mwamba.

Sambamba na kushindwa huko, Waziri Sitta pia amejikuta katika wakati mgumu, baada ya kuachwa mpweke na maswahiba wake wa kisiasa ambao amekuwa akiwatangaza kuwa ni waadilifu wa mfano wake wanaostahili kukabidhiwa dhamana ya uongozi wa juu wa taifa, ambao walishindwa kutokea katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa Katoliki la Parokia ya Ilumya iliyopo wilayani Busega, mkoani Mwanza.

Katika harambee hiyo ambayo, Sitta alikuwa mgeni rasmi, alikusudiwa kuchangisha kiasi cha shilingi milioni 217, jambo ambalo alishindwa kulitimiza na kujikuta akifanikiwa kuchangisha fedha tasilimu pamoja na ahadi shilingi milioni 9.3 huku yeye binafsi akichangia shilingi milioni tatu.

Katika harambee hiyo, wanasiasa wengine wenye majina makubwa waliokuwa wamealikwa ambao Waziri Sitta amekuwa akiwataja kuwa ni washirika wake wa kisiasa, ni pamoja na Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, Waziri wa Uchukuzi, Harrison Mwakyembe na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bernard Membe.

Hata hivyo, mawaziri hao hawakuhudhuria hafla hiyo na Waziri Sitta alieleza kuwa walikosa nafasi ya kufika Mwanza wala kuwasilisha michango yao huku akitoa ahadi kuwa watafika na michango wakati Rais Jakaya Kikwete atakapofanya ziara katika Mkoa wa Simiyu.

Kauli hiyo ya Waziri Sitta iliibua minong’ono miongoni mwa waalikwa, waliohoji sababu ya kuwepo kwa matangazo mengi ya ujio wa Mawaziri hao kuungana na Sitta na hata kushindwa kuwasilisha michango yao.

Hayo yametokea ikiwa ni siku chache baada ya Sitta kukaririwa akihoji hatua ya baadhi ya wanasiasa kushiriki kuchangisha mamilioni ya fedha katika harambee za ujenzi wa makanisa na misikiti sehemu mbalimbali hapa nchini.

Sitta ambaye kwa muda mrefu sasa anafahamika na wengi hapa nchini kuwa ni mpiganaji vita dhidi ya ufisadi, katika kile kilichoonekana kuwa ni kuwashambulia hao aliohoji hatua ya kuchangisha fedha katika nyumba za ibada, pia alionekana kushangazwa na marafiki ambao wamekuwa wakitajwa kwenye matukio hayo kuchangia mamilioni ya fedha na kutaka jamii ijulishwe walipo.

Baadhi ya waumini walioshiriki harambee hiyo walizungumzia na  kuhusu kutoonekana kwa mawaziri, walisema ni jambo la kushangaza kwani hata taarifa za kutofika kwao hazikutolewa mapema, hivyo wananchi wengi walifika kwenye shughuli hiyo wakiwa na matumaini ya kuwaona viongozi hao.

Viongozi walioungana na Sitta katika harambee hiyo ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Paschal Mabiti aliyechangia Sh 500,000 huku ofisi yake ikichangia Sh milioni moja.

Wengine ni Mbunge wa Busega, Titus Kamani, ambaye alichangia Sh 500,000, mfanyabiashara Emmanuel Gungu milioni moja na mifuko 50 ya saruji.

*Aanguka vibaya harambee ya kanisa Busega
*Magufuli, Membe na Mwekyembe wakwama

HARAKATI za Waziri wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta, kufanya kile ambacho kimekuwa kikifanywa na wanasiasa wa kariba yake ambao amekuwa akiw
ashambulia kwa kujihusisha na masuala ya kijamii, zimegonga mwamba.

Sambamba na kushindwa huko, Waziri Sitta pia amejikuta katika wakati mgumu, baada ya kuachwa mpweke na maswahiba wake wa kisiasa ambao amekuwa akiwatangaza kuwa ni waadilifu wa mfano wake wanaostahili kukabidhiwa dhamana ya uongozi wa juu wa taifa, ambao walishindwa kutokea katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa Katoliki la Parokia ya Ilumya iliyopo wilayani Busega, mkoani Mwanza.

Katika harambee hiyo ambayo, Sitta alikuwa mgeni rasmi, alikusudiwa kuchangisha kiasi cha shilingi milioni 217, jambo ambalo alishindwa kulitimiza na kujikuta akifanikiwa kuchangisha fedha tasilimu pamoja na ahadi shilingi milioni 9.3 huku yeye binafsi akichangia shilingi milioni tatu.

Katika harambee hiyo, wanasiasa wengine wenye majina makubwa waliokuwa wamealikwa ambao Waziri Sitta amekuwa akiwataja kuwa ni washirika wake wa kisiasa, ni pamoja na Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, Waziri wa Uchukuzi, Harrison Mwakyembe na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bernard Membe.

Hata hivyo, mawaziri hao hawakuhudhuria hafla hiyo na Waziri Sitta alieleza kuwa walikosa nafasi ya kufika Mwanza wala kuwasilisha michango yao huku akitoa ahadi kuwa watafika na michango wakati Rais Jakaya Kikwete atakapofanya ziara katika Mkoa wa Simiyu.

Kauli hiyo ya Waziri Sitta iliibua minong’ono miongoni mwa waalikwa, waliohoji sababu ya kuwepo kwa matangazo mengi ya ujio wa Mawaziri hao kuungana na Sitta na hata kushindwa kuwasilisha michango yao.

Hayo yametokea ikiwa ni siku chache baada ya Sitta kukaririwa akihoji hatua ya baadhi ya wanasiasa kushiriki kuchangisha mamilioni ya fedha katika harambee za ujenzi wa makanisa na misikiti sehemu mbalimbali hapa nchini.

Sitta ambaye kwa muda mrefu sasa anafahamika na wengi hapa nchini kuwa ni mpiganaji vita dhidi ya ufisadi, katika kile kilichoonekana kuwa ni kuwashambulia hao aliohoji hatua ya kuchangisha fedha katika nyumba za ibada, pia alionekana kushangazwa na marafiki ambao wamekuwa wakitajwa kwenye matukio hayo kuchangia mamilioni ya fedha na kutaka jamii ijulishwe walipo.

Baadhi ya waumini walioshiriki harambee hiyo walizungumzia na kuhusu kutoonekana kwa mawaziri, walisema ni jambo la kushangaza kwani hata taarifa za kutofika kwao hazikutolewa mapema, hivyo wananchi wengi walifika kwenye shughuli hiyo wakiwa na matumaini ya kuwaona viongozi hao.

Viongozi walioungana na Sitta katika harambee hiyo ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Paschal Mabiti aliyechangia Sh 500,000 huku ofisi yake ikichangia Sh milioni moja.

Wengine ni Mbunge wa Busega, Titus Kamani, ambaye alichangia Sh 500,000, mfanyabiashara Emmanuel Gungu milioni moja na mifuko 50 ya saruji.
Download Our App

1 comments:

USIIGE TEMBO KUNYA UTAPASUKA MSAMBA NI HIVI HIVI ASKOFU MMOJA AMBAYE NI MAREHEMU SI VEMA KUMTAJA ALITUHUMIWA KWA UFISADI ALIPOSTUKIWA AKAPATA STROKE AKAELEKEA KUZIMU ILA ILE KAULI YA KUKU KUDANGANYA VIFARANGA KUWA WATANYONYA KESHO VIFARANGA WAMESTUKA WANATAKA KUNYONYA LEO IWAPO KATIKA ENZI HIZI ZA UCHUMI HURIA UKISHINDWA COMPETITION NI VEMA UNYAMAZE USITAKE UHURUMIWE IKIZINGATIA MFUMO WA UBEPARI HAKUNA REFA NI VEMA UKIONA MWENZAKO ANAKUSANYA KWA CHEPE UTAKUWA MWEHU KUKUSANYA KWA KIJIKO NDIO SOKO HURIA UNGANA NA MABEPARI WENZIO MUKABILI USHINDANI UKISHINDWA NYAMAZA KAWAIDA MABEPARI HUUNGANA HAKUNA UJAMAA TENA ACHA NDOTO

Reply

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top