Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

LEMA AIKABA KOO POLISI

Photo: Lema aing’ng’ania polisi bomu la Soweto Arusha

Arusha. Mbunge wa Arusha, Godbless Lema, ameendelea kushikilia madai yake kuwa polisi wanahusika na tukio la bomu lililolipuka  katika mkutano wa kampeni ya chama hicho Viwanja vya Soweto  Arusha na kusababisha vifo vya watu wanne.

Lema alitoa madai hayo juzi alipohutubia mkutano wahadhara Viwanja vya Shule ya Msingi Ngarenaro.

Alidai Rais Jakaya Kikwete amegoma kuunda tume huru ya kimahakama kuchunguza tukio hilo, ili kunusuru  polisi na aibu ya kushiriki uhalifu na mauaji ya raia wasio na hatia.

“Mauaji ya Soweto yalipangwa na kutekelezwa na  polisi, RPC (Kamanda wa Polisi) wa Arusha anajua mpango mzima ndiyo maana Rais hataki kuunda tume kama Chadema tulivyomuomba, ili tuwasilishe ushahidi wa video kuonyesha jinsi walivyohusika,” alisema Lema

Alisema ushindi wa Chadema kata nne za Elerai, Kimandolu, Themi na Kaloleni ni dalili njema za ushindi kwa nafasi zote kuanzia udiwani, ubunge na urais Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.

Naye Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa, alitaka polisi kukitambua na kukiheshimu Chadema na viongozi wake,  kwa sababu ni chama kilichoundwa na kuongozwa kwa kuzingatia katiba na sheria za nchi.

“Hatutakubali kuonewa, kunyanyaswa wala kupuuzwa kwa sababu iwayo yote,” alisema Golugwa.

Alishukuru  ulinzi wa Mungu mlipuko wa bomu, ushindi na walitangaza kuanza vikao vya  katiba leo.
Arusha. Mbunge wa Arusha, Godbless Lema, ameendelea kushikilia madai yake kuwa polisi wanahusika na tukio la bomu lililolipuka katika mkutano wa kampeni ya chama hicho Viwanja vya Soweto Aru
sha na kusababisha vifo vya watu wanne.

Lema alitoa madai hayo juzi alipohutubia mkutano wahadhara Viwanja vya Shule ya Msingi Ngarenaro.

Alidai Rais Jakaya Kikwete amegoma kuunda tume huru ya kimahakama kuchunguza tukio hilo, ili kunusuru polisi na aibu ya kushiriki uhalifu na mauaji ya raia wasio na hatia.

“Mauaji ya Soweto yalipangwa na kutekelezwa na polisi, RPC (Kamanda wa Polisi) wa Arusha anajua mpango mzima ndiyo maana Rais hataki kuunda tume kama Chadema tulivyomuomba, ili tuwasilishe ushahidi wa video kuonyesha jinsi walivyohusika,” alisema Lema

Alisema ushindi wa Chadema kata nne za Elerai, Kimandolu, Themi na Kaloleni ni dalili njema za ushindi kwa nafasi zote kuanzia udiwani, ubunge na urais Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.

Naye Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa, alitaka polisi kukitambua na kukiheshimu Chadema na viongozi wake, kwa sababu ni chama kilichoundwa na kuongozwa kwa kuzingatia katiba na sheria za nchi.

“Hatutakubali kuonewa, kunyanyaswa wala kupuuzwa kwa sababu iwayo yote,” alisema Golugwa.

Alishukuru ulinzi wa Mungu mlipuko wa bomu, ushindi na walitangaza kuanza vikao vya katiba leo.

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top