Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimina na Balozi wa Kenye nchini Tanzania, Mutiso Mutinda, wakati
alipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 20,
2013 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Kenya nchini Tanzania aliyemaliza
muda wake, Mutiso Mutinda, wakati Balozi huyo alipofika Ofisini kwa
Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kumuaga baada ya
kumaliza muda wake wa kazi nchini. Kushoto ni Kaimu Balozi wa Kenya,
Peter Sang. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPO CHINI
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Kenya nchini Tanzania aliyemaliza
muda wake, Mutiso Mutinda, aliyeongozana na ujumbe wake wakati Balozi
huyo alipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti
20, 2013 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi
nchini.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akipokea Kitabu cha Kamusi ya Kiswahili, kutoka kwa balozi wa
Kenya nchini Tanzania aliyemaliza muda wake, Mutiso Mutinda, wakati
Balozi huyo alipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam leo
Agosti 20, 2013 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi
nchini. Kushoto ni Kaimu Balozi wa Kenya, Peter Sang. Kitabu hicho
kimetungwa na Balozi huyo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Kenya nchini Tanzania,
aliyemaliza muda wake, Mutiso Mutinda, na ujumbe wake baada ya
mazungumzo yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam,
leo. Balozi huyo alifika kwa ajili ya kumuaga Makamu baada ya kumaliza
muda wake wa kazi nchini.
******************************************
MAKAMU WA RAIS AAGANA NA BALOZI WA KENYA NCHINI TANZANIA
JUMANNE 20, 2013
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal
leo ameagana rasmi na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mheshimiwa Balozi
Mutiso Mutinda. Shughuli hiyo ya kuagana imefanyika ofisini kwa
Mheshimiwa Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo Balozi
Mutiso amemueleza Mheshimiwa Makamu wa Rais kuwa, amefurahi kufikia
kikomo cha utumishi wake kama Balozi nchini Tanzania na kwamba siku zote
alizokuwa akifanya kazi hapa nchini ziliambatana na furaha kufuatia
kuishi katika nchi yenye amani tele na watu wakarimu na wanaoheshimu utu
wa watu.
Balozi
Mutiso alisema katika kipindi chake hapa Tanzania uhusiano baina ya
Kenya na Tanzania umeimarika zaidi na kwamba pale Kenya ilipohitaji
msaada wa aina yoyote Tanzania imekuwa rafiki na jirani mwema.
“Nashukuru sana Mheshimiwa Makamu wa Rais kwa kunipa fursa ya kuja
kuagana nawe.
Kwa
kweli umekuwa kiongozi wa karibu nami na kwamba katika kipindi ambacho
nimekuwa Tanzania mengi yamefanyika ambayo yanaashiria kuimarika kwa
uhusiano baina ya nchi zetu. Ni wazi kuwa mengi yataendelea kufanyika
hata katika kipindi ambachio nitakuwa nje ya hapa,” alisema.
Balozi
Mutiso ambaye pia katika kazi nyingine alizofanya amefanikiwa kuandika
Kamusi ya Diplomasia, alimkabidhi Kamusi hiyo ambayo imechapishwa na
TUKI na kisha kufafanua kuwa, Kamusi hiyo itakuwa chagizo la kuongeza
ari ya uzungumzaji wa lugha ya Kiswahili katika nchi za Afrika
Mashariki.
Kwa
upande wake Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal mara baada ya kupiokea Kamusi hiyo
alimtaja Balozi Mutiso kama Balozi mfano wa kuigwa kutokana na kutumia
nafasi yake vema kuimarisha mahusiano baina ya Kenya na Tanzania.
Mheshimiwa
Makamu wa Rais alieleza kuwa, katika kipindi Balozi Mutiso akiwa nchini
Kenya imefanikiwa kutanua uwekezaji katika Tanzania na kwamba uhusiano
wa kiuchumi baina ya nchi hizi mbili umeimarika zaidi jambo analotarajia
kuwa litazidi kuendelea hata wakati ambapo Balozi Mutiso atakuwa katika
majukuimu mengine.
“Nakupongeza kwa kazi nzuri uliyofanya na nakutakia mafanikio zaidi katika majukumu mapya utakayopangiwa,” alisema
Mheshimiwa
Makamu wa Rais huku akimuahidi Balozi Mutiso kuwa kazi nzuri
aliyoifanya atahakikisha kuwa inaendelea hasa katika eneo la utunzaji
mazingira.
Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
Ikulu, Dar es Salaam
Post a Comment