Na Mwandishi Wetu
Taasisi
ya Urejesho wa Maadili ya Taifa (Taumata) iliyosajiriwa kwa usajiri
namna S.A 18827, imesisistiza kuwa kurejea katika maadili mema ndio
ufumbuzi wa matatizo yanayolikabili Taifa kwa sasa nasio vinginevyo.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es salaam mkurugenzi wa Taasisi ya
urejesho wa maadili ya Taifa ndugu Joseph Goliama alisema kutoka katika
maadili mabaya na kuingia katika maadili mema ndio ufumbuzi wa matatizo
ya Taifa kwasasa
Alisema
kuwa makundi mbalimbali ya wananchi kuacha maadili mema ya Taifa ndio
kumekuwa msingi chanzo na kiini cha Taifa kupoteza Sauti moja ya
kuisikiliza na mwelekeo mmoja wa kuufuata hali inayosababisha makundi
mbalimbali ya wananchi kutokuwa na amani kutopendana na kutokuaminiana
Goliama
alisema kuwa maadili mabaya ambayo yanafanya Taifa kupoteza amani, umoja
na mawasiliano ni pamoja na makundi mbalimbali ya wananchi kuwaziana
mabaya, kutazamiana mabaya, kuneneana maneno mabaya, kutendeana mabaya,
kuonana kwa jicho baya,kuhusiana kwa uhusiano mbaya, kufanyiana maamuzi
yasiyo ya haki na kusimamiana kwa misimamo isiyo ya haki
Tunawashauri
watanzania wa makundi yote kurudi katika maadili mema na kuacha maadili
mabaya ambayo yanatishia ustawi na maendeleo ya Taifa letu alisema
Goliama
Alitoa
mfano na kusema maadili mabaya ndio yametumbukiza mataifa mengi katika
vita vya wenyewe kwa wenyewe hivyo akawataka wananchi wa makundi yote
kulinda na kutetea maadili mema ambayo yameifanya Tanzania kuitwa kisiwa
cha amani
Aliitaka
serikali kuangalia uwezekano wakuyakutanisha makundi yote ya wananchi
nakuyakalisha pamoja ili yakubaliane ni Taifa gani yanataka kulijenga
litakalohakikishia kila kundi ustawi na maendeleo endelevu .
Akifafanua
zaidi alisema wadau wa amani na umoja wa Taifa ni wananchi wa makundi
yote yakiwemo makundi ya dini, vyama vya siasa, jinsia, rika,
wafanyabiashara, wafugaji, wakulima, wafanya kazi ,Askari nakuyataka
makundi hayo kupigania amani na umoja na haki ili Taifa liapate ustawi
na maendeleo endelevu.
Goliama
alimalizia kwa kuitaka serikali iishirikishe taasisi ya urejesho wa
maadili ya Taifa katika majukum yake ya kutafuta amani ,umoja na
mshikamano wa kitaifa :CHANZO Majuto Omary
Post a Comment