Helikopta
maalum iliyowabeba viongozi wa CHADEMA akiwemo Mwenyekiti wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Jimbo la Hai, Mh. Freeman
Mbowe pamoja na Mbunge wa jimbo la Ubungo Mh. John Mnyika walipowasili
eneo la Mnada Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza kufanya mkutano wa
hadhara wilayani humo mwishoni mwa Juma. (Picha na Zainul Mzige wa Dewji Blog).
Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Jimbo la
Hai, Mh. Freeman Mbowe akihutubia wakazi wa wilaya ya Sengerema Mkoa wa
Mwanza mwishoni mwa juma kwenye mkutano wa hadhara. (Picha na Zainul
Mzige wa Mo Blog).
Mwananchi wa Geita ambaye jina lake halikuweza kupatikana kiurahisi akitoa maoni yake ya Rasimu ya Katiba Mpya mbele
umati wa wafuasi wa Chadema na wakazi wa wilaya hiyo ambapo wengi wao
wametaka Ushuru wa Masoko ufutwe pamoja na baadhi ya kinamama
kulalamikia shida ya Maji kwenye Wilaya hiyo na Mh.Mbowe aliwaasa kutumia Mabaraza ya CHADEMA kuwasilisha maoni yao wakati wa mkutano wa hadhara.
Mbunge
wa Jimbo la Ubungo Mh. John Mnyika akiteta jambo na mmoja wa viongozi
wa Chadema wilayani Sengerema Hemedi Sabula wakati wa mkutano huo wa
hadhara.
Na Mwandishi wetu.
Mwenyekiti
wa Chama cha Domekrasia na maendeleo (CHADEMA) Mh.FREEMAN MBOWE
amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kujadili Rasimu ya Katiba mpya
ili ipatikane Katiba itakayokidhi haja ya Watanzania.
Amesema
hayo alipokuwa akiwahutubia wakazi wa wilaya ya Sengerema mkoani
waMwanza alipokuwa kwenye ziara ya kichama kuhamasisha wanachama wa
chama hicho kuunga mkono kuwepo na Serikali tatu ndani ya Jumuiya ya
Muungano wa Tanzania.
Amesema
kuwepo Serikali tatu siyo mzigo kama Chama cha Mapinduzi (ccm)
kinavyosema ila tunataka kuwepo serikali ya Tanganyika na Zanzibari na
ile ya muungano ili kuleta usawa ndani ya Muungano huo.
Pia
amesema kuwa Lugha ya Kiingereza na Kiswahili ipatiwe kipaumbele
kufundishwa kuanzia daraja la awali hadi Chuo Kikuu ili kuwajengea
Watanzania kufahamu Lugha ya Kiingereza vema na kupata ajira kwa
urahisi.
Post a Comment