Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mtwara imemfutia shtaka la kesi
ya uchochezi iliyokuwa inamkabili Mbunge wa Mtwara Mjini (CCM)Hasnein
Murji .
Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa upande wa
utetezi, Peter Kibatala kuiomba mahakama kuifuta kesi hiyo iliposomwa
Julai 3, mwaka huu kwa madai ya kuwa hati ya mashtaka ni dhaifu kisheria
na haionyeshi ni makosa yapi mtuhumiwa aliyotenda.
Wakili Kibatala alieleza mahakama kuwa kifungu cha
129 na 132 cha sheria ya mwenendo wa makosa jinai ni lazima mshtakiwa
aelezwe mashtaka yake wazi wazi yanayomkabili.
Murji alifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani
hapo akikabiliwa na kesi ya uchochezi anayodaiwa kuifanya Januari
19,mwaka huu katika eneo la Ligula mkoani hapa.
Hakimu Mkazi Mfawidhi Dynes Lyimo alifuta shtaka
hilo na kumwachia mshtakiwa huru baada ya kesi hiyo kuahirishwa tangu
Julai 3,mwaka huu. Wakati huo huo viongozi wa upinzani Katani Ahmed
Katani (33) na Saidi Kulaga (45) wa CUF wanaokabiliwa na mashtaka matatu
ya kula njama, kufanya uchochezi na kuamsha hisia mbaya kwa wakazi wa
Jamhuri wamefikishwa mahakamani. MWANANCHI
Post a Comment