Mechi
hiyo ya Ngao ya Jamii (Community Shield) kuashiria ufunguzi wa msimu
mpya wa 2013/2014 iliyochezwa jana (Agosti 17 mwaka huu) Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 208,107,000. Washabiki 26,084
walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo ilimalizika kwa Yanga
kushinda Azam bao 1-0.
Mgawanyo
wa mapato ya mechi hiyo uliokuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 31,745,135.59, asilimia 10 ya mchango wa
kusaidia jamii sh. 20,810,700, gharama ya tiketi sh. 7,309,866.
Uwanja
sh. 22,236,194.76, gharama za mchezo sh. 13,341,716.86, Chama cha Mpira
wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 5,188,445.44, TFF sh.
13,341,716.86 na Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
6,670,858.43. Kila klabu imepata mgawo wa sh. 43,731,183.03.
Post a Comment